Na. Antonia Mbwambo -Dodoma
Tarehe 15
Januari, 2026
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi ametoa wito kwa baadhi ya wakurugenzi wa Idara za Ofisi yake pamoja na Ofisi ya Rais, Katiba Sheria na Utawala Bora ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuleta mageuzi na kujenga Utumishi wa Umma uliotukuka kwa ustawi wa Taifa.
Bw. Daudi ameyasema hayo leo
tarehe 15 Januari, 2026 wakati akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI
Bw. Juma Mkomi katika kikao cha kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa majukumu
ya kiutumishi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo uliyopo Mtumba jijini
Dodoma.
“Ili kujenga na kuboresha Utumishi
wa Umma wenye tija ni vizuri tukashirikiana wenyewe kwa wenyewe hasa kwa yale
mazuri tuliyo nayo ndani ya muungano” Bw. Xavier alisema.
Nae Naibu Katibu Mkuu Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bw. Omar Haji Gora ameushukuru uongozi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI chini ya Katibu wake Mkuu Bw. Juma Mkomi kwa Kuwaonesha ushirikiano kila wakati na kuahidi kuwa yale yote waliyojifunza wataenda kuyafanyia kazi ili kuleta mageuzi katika Utumishi wa Umma.
“Tumepata faraja kuwa hapa, na yale
ambayo tumejifunza tunaenda kuyafanyia kazi ili kuendelea kujenga utumishi wa
umma ulio Bora” Bw. Gora alisema.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi akizungumza
na wakurugenzi wa Idara za Ofisi yake pamoja na Viongozi kutoka Ofisi ya Rais,
Katiba Sheria na Utawala Bora ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kikao
cha kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi kilichofanyika
katika ukumbi wa Ofisi hiyo uliyopo Mtumba jijini Dodoma
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.
Xavier Daudi (hayupo pichani) kikao cha kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa
majukumu ya kiutumishi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo uliyopo
Mtumba jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Utumishi na Utawala
Bora Bw. Omar Haji Gora akitoa neno la shukrani kwa Uongozi wa Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora baada ya kuhitimisha kikao
cha kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi kilichofanyika
leo tarehe 15 Januari, 2026 katika
ukumbi wa Ofisi hiyo uliyopo Mtumba jijini Dodoma
Sehemu ya Washiriki kutoka Ofisi
Kuu ya Utumishi wa Umma Zanzibar wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi (hayupo
pichani) akizungumza nao katika kikao cha kubadilishana uzoefu wa utekelezaji
wa majukumu ya kiutumishi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo uliyopo
Mtumba jijini Dodoma
Sehemu ya washiriki wa kikao cha
kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi wakisikiliza
fafanuzi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) katika kikao
cha kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi kilichofanyika
katika ukumbi wa Ofisi hiyo uliyopo Mtumba jijini Dodoma
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.
Xavier Daudi (hayupo pichani) katika kikao cha kubadilishana uzoefu wa
utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo
uliyopo Mtumba jijini Dodoma
Sehemu ya washiriki wa kikao cha
kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi wakisikiliza wakimsikiliza
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) katika kikao cha kubadilishana uzoefu wa
utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo
uliyopo Mtumba jijini Dodoma



No comments:
Post a Comment