Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 05 Januari, 2026
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus Kapinga amewakumbusha
Watumishi wa ofisi hiyo kuongeza ufanisi na uwajibikaji kwa Mwaka 2026 ili
kutimiza malengo waliyojiwekea kwa maslahi mapana ya Taifa.
Bw. Kapinga ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa
ofisi hiyo katika eneo maalum la mafunzo
kwa watumishi hao kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa wa masuala mbalimbali
ya kiutumishi ambayo hufanyika kila siku ya Jumatatu Mtumba Jijini Dodoma.
Bw. Kapinga amewasisitiza Watumishi hao
kushirikiana kutekeleza majukumu yao ili kufikia malengo waliyojiwekea katika kutoa huduma bora
kwa kila Mtanzania.
“Mwaka uliopita 2025 tulitekeleza majukumu
yetu vema na kutimiza malengo tuliyojiwekea, natoa rai kwa mwaka 2026 tushirikiane
pia katika kutekeleza majukumu yetu ili Wadau na
Wananchi wetu wanufaike na huduma tunazozitoa” alisisitiza
Bw. Kapinga.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo Bw. Mosses Raymond amesema Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora ina majukumu mengi ikiwemo utoaji wa huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, ni muhimu kila mtumishi akajua wajibu wake ili huduma zitakazotolewa kwa Watumishi wa Umma na Wananchi ziwe zenye manufaa.
Aidha Bw. Raymond amesema, ili kuilinda taswira nzuri ya ofisi hiyo ni vizuri kila mtumishi kuendelea kuwa mwadilifu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma wanapokuwa ndani au nje ya ofisi.
Kadhalika Bw. Raymond amewapongeza Watumishi wa ofisi hiyo kuwasili kwa wakati katika maeneo yao ya kazi jambo linaloonyesha kwamba kila mmoja anajua wajibu wake na kufurahia mazingira wanayofanyia kazi.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw.
Cyrus Kapinga akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha
utendaji kazi
watumishi wa ofisi hiyo yanayofanyika kila Jumatatu kwenye Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mwezeshaji wa mafunzo, Bw. Mosses Raymond akiwasilisha
mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo
na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo yanayofanyika kila
Jumatatu kwenye Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi
ya Rais-UTUMISHI
na Utawala Bora, wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji
kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo
iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi
ya Rais-UTUMISHI
na Utawala Bora, wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji
kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo
iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI
na Utawala Bora, wakiwa
kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo
iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI
na Utawala Bora, wakifuatilia
jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji
kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo
iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Uzingatiaji wa Maadili,
Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Janet Mishinga akikata keki ya
kuukaribisha Mwaka Mpya kwa niaba ya Watumishi wote wa ofisi hiyo mara baada ya
kumaliza mafunzo ya
kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa
Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Maafisa wa ofisi hiyo.
No comments:
Post a Comment