Na Antonia Mbwambo-Arusha
Tarehe 9 Januari, 2026
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Regina Qwaray amesisitiza
waratibu wa miradi ya TASAF kwa kushirikiana na kaya nufaika kulinda miradi
dhidi ya waharifu wa miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa manufaa ya walengwa
na taifa kwa jumla.
Mhe. Qwaray ameyasema hayo leo
Januari 9, 2026 alipokuwa akizungumza na waratibu, wasimamizi na wanufaika wa miradi
ya TASAF Mkoani Arusha.
Mhe. Qwaray amewapongeza TASAF
kwa taarifa nzuri ya ujenzi wa shule ya sekondari Oldonuwas iliyopo kijiji cha
Oldonuwas na ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji uliopo Meru kijiji cha Ngabobo
wilaya ya Meru.
“Nimesikiliza taarifa zenu na
nimejionea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo yenye manufaa kwa
wanufaika wa TASAF na taifa kwa jumla, hivyo nitoe rai ya kuilinda na kuithamini
ili tupate tija iiyokusudiwa na Serikali” alisema Mhe. Qwaray.
Aliongeza kuwa, Rais wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha
nyingi ili kuhakikisha watanzania hasa kaya maskini zinanufaika kupitia TASAF. Hivyo,
amewaomba wananchi wa wanaozunguka miradi hiyo kuwa walinzi ili miradi hiyo iweze
kunufaisha vizazi vya sasa na vile vijavyo.
Aidha, Mhe. Qwaray amesema
kuwa miradi ya TASAF ni chachu ya maendeleo kwa kuwa watanzania hasa wanaotoka
katika kaya maskini wanajikwamua kutoka katika wimbi la umaskini kwa kupata
elimu kutokana na ujenzi wa shule na wananufaika na mfereji wa umwagiliaji kwa
kufanya kilimo cha mahindi, nyanya, vitunguu na maji kwa ajili ya mifugo.
Naibu Waziri,Ofisi yas Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, mhe. Regina Qwaray (wa pili kulia) akiwa anapewa maelezo ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa shule ya Oldnuwas na Mkurugenzi wa Hamashauri ya wilaya ya Arusha Bw. Seleman Msumi wakati wa ziara yake ya kikazi iliyofanyika mkoani Arusha leo tarehe 9 January, 2026.
Timu ya wataalam kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa na Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru wakioongozana na Naibu
Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, mhe.
Regina Qwaray kukagua mradi wa TASAF wa shule ya sekondari Oldonuwas iliyopo kijiji
cha Oldonuwas jijini Arusha leo Januari 9, 2026.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Oldonuwas wanaonufaika na mradi wa TASAF wa ujenzi wa shule ya sekondari Oldnuwas wakimsikiliza Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akizungumza nao baada ya kuwasili kijijini hapo kuona maendeleo ya miradi hiyo leo tarehe 9 Januari, 2026 jijini Arusha
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ambaye ni Afisa
Miradi TASAF Bw.Agustino Ngude akitoa neno la Utangulizi kwa Naibu Waziri,Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, mhe. Regina Qwaray
kabla ya kupokea Taarifa ya maendeleo ya wa Mradi wa TASAF wa shule ya
sekondari Oldonuwas iliyopo kijiji cha Oldonuwas na ujenzi wa mfereji wa
umwagiliaji uliopo Meru kijiji cha Ngabobo wilaya ya Meru jijini Arusha
Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, mhe. Regina Qwaray (aliyevaa suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya viongozi wa Mkoa wa Arusha kabla ya kutembelea Mradi wa TASAF wa ujenzi wa shule ya sekondari Oldonuwas iliyopo kijiji cha Oldonuwas na ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji uliopo Meru kijiji cha Ngabobo wilaya ya Meru.
sehemu ya wananchi ambao ni wanufaika wa mradi wa TASAF wa ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji uliopo Meru kijiji cha Ngabobo wilaya ya Meru jijini Arusha wakimsikiliza Naibu Waziri,Ofisi yas Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, mhe. Regina Qwaraywakati alipofika kukaguia mradi huo tarehe 9 Januari,2026Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, mhe. Regina Qwaray pamoja na timu waliyoongozana nayo
wakikagua maendeleo ya ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji uliopo Meru kijiji cha
Ngabobo wilaya ya Meru jijini Arusha ambao umekuwa ukiwanufaisha wananchi
katika undeshaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kijijini hapo.
No comments:
Post a Comment