Na. Veronica Mwafisi na Antonia Mbwambo-Dar es salaam
Tarehe 23
Januari, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ni muhimu kwa Taasisi ya UONGOZI kuendelea kuwaandalia program za Uongozi Watumishi wa Umma wenye mwelekeo wa Uongozi leadership potential ili kuwa na Viongozi watakaokuwa na uzalendo na weledi katika taifa.
Waziri Kikwete ameyasema hayo leo tarehe 23 Januari, 2026 jijini Dar es salaam alipotembelea taasisi hiyo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mhe. Kikwete amesema, uamuzi
wa kushirikisha wafanyakazi wa Taasisi za Umma, binafsi na za kiraia katika program hizo unatoa fursa kwa
washiriki hao kubadilishana uzoefu na kuboresha utendaji.
Amesema ni wakati sahihi
wa kuweka mikakati ya ujenzi wa Kituo cha Uongozi (Leadership Center) ambacho zaidi kitawajengaViongozi katika Utumishi wa
Umma.
Akihitimisha hotuba
yake Mhe. Kikwete ameipongeza Menejimenti na Watumishi wote wa Taasisi ya
Uongozi kwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Kwa upande
wake, Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua katika nafasi ya Naibu Waziri wa
Ofisi hiyo ambapo ameomba ushirikiano Ili kwa pamoja waweze kumsaidia Rais
katika kutekeleza majukumu ya Utumishi na Utawala Bora.
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi yake, aliwashukuru Viongozi hao kwa kuwatembelea na kuhimiza uwajibikaji na kuahidi kuyafanya kazi maelekezo watakayopewa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete (katikati) akiteta jambo na Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Mahendeka (kushoto)
baada ya Waziri huyo kuzungumza na watumishi wa Taasisi ya UONGOZI wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji. Kulia
ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi
ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akimuonesha
kitabu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) wakati Waziri huyo alipokuwa
akipitishwa kwenye baadhi ya Idara za Taasisi hiyo wakati Waziri huyo
alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji. Kushoto ni Naibu Waziri wake
Mhe, Regina Qwaray.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya UONGOZI
jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji. Wa pili kulia waliokaa ni Naibu Waziri wake, Mhe. Regina
Qwaray na wa pili kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu-IKULU Bw. Mululi Mahendeka.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa
ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.
Sehemu ya Watumishi wa Taasisi ya UONGOZI
jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga
kuhimiza uwajibikaji.
Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Mahendeka akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Regina Qwaray ili amkaribishe Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza kulia) kwa ajili ya kuzungumza na Watumishi wa Taasisi ya UONGOZI wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.
Sehemu ya Watumishi wa Taasisi ya UONGOZI wakifuatilia
wasilisho la taarifa ya
utekelezaji wa taasisi hiyo iliyowasilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Bw. Kadari Singo (hayupo pichani) wakati
wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment