Tuesday, January 6, 2026

WAZIRI KIKWETE AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE NA MAMA ANNA MKAPA

Na. Veronica Mwafisi-Dar es salaam

Tarehe 06 Januari, 2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewatembelea na kuwajulia hali Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam na Mama Anna Mkapa, mke wa Hayati Benjamin William Mkapa nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo Januari, 2026.

Mhe. Kikwete amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anathamini sana mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliomtangulia na ataendelea kusimamia na kutunza familia hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizowekwa.

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema, kuwatembelea na kuwajulia hali wake hao wa Viongozi Wastaafu ni moja ya majukumu yake ambayo anayatekeleza kwa lengo la kuwajulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizowekwa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema ofisi hiyo itafanyia kazi maoni na ushauri uliotolewa na wajane hao.

Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Mhe. Kikwete kwa kupata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali na amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake wakati wote pasipo kuchoka.

Naye, Mama Anna Mkapa ameishukuru ofisi hiyo kwa kufuatilia kwa karibu masuala yanayowahusu na kuyatafutia ufumbuzi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Mama Maria Nyerere (wa kwanza kulia), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mama Maria Nyerere (kulia), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. 


Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kushoto) alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Mama Maria Nyerere (hayupo pichani), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi



Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Dawati la Viongozi wa Kitaifa Wastaafu, Bi. Nyasinde Mukono (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo wakati Mama Maria Nyerere (hayupo pichani), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokuwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipomtembelea kumjulia hali. Wengine ni Wakurugenzi kutoka katika ofisi hiyo.

Wakurugenzi na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakiwa nje ya nyumba ya Mama Maria Nyerere 9hayupo pichani), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kumjulia hali Mama Maria ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akifurahia jambo na Mama Anna Mkapa (kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa wakati alipomtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akifafanua jambo kwa Mama Anna Mkapa (hayupo pichani), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye alimtembelea Mama Anna Mkapa kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026.


Mama Anna Mkapa (wa kwanza kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa akimsindikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) wakati Waziri huyo akiondoka baada ya kumtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiagana na Mama Anna Mkapa (kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa wakati alipomtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akiagana na Mama Anna Mkapa (wa kwanza kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) kumtembelea Mama Anna Mkapa nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mama Anna Mkapa (katikati), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Januari, 2026.  Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi na wengine ni Wakurugenzi kutoka katika ofisi hiyo.







No comments:

Post a Comment