Na. Mwandishi Wetu-Dar es Salaam
Tarehe: 17 Januari, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) ametoa wito kwa wasimamizi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) kujitangaza, kutoa elimu na kubuni njia bora zenye ushawishi ambazo zitawezesha mfuko kupata wawekezaji zaidi ambao watakuza mtaji.
Mhe. Kikwete ametoa wito huo Januari 17, 2026
wakati akifungua Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa
Wawekezaji wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) uliofanyika jijini Dar
es Salaam.
Katika hotuba yake, ameipongeza
Bodi, Menejimenti na Watumishi wote wa WHI kwa kufanikisha ukuaji wa Mfuko na thamani ya kipande. Alifafanua kuwa
hadi kufikia tarehe 30 Juni 2025, ukubwa wa Mfuko uliongezeka hadi kufikia Shilingi
bilioni 43.99 sawa na ongezeko la asilimia 69 kutoka Shilingi bilioni 25.97
zilizonakiliwa kipindi kilichoishia Juni 2024.
Aliongeza kuwa, ongezeko hilo lilihusisha pia
kuongezeka kwa thamani halisi ya kipande kilichoongezeka kwa shilingi 16.86
kutoka shilingi 115.812 hadi shilingi 132.6730 sawa na pato la asilimia 14.6
kwa mwaka.
“Leo tunapata fursa ya kupokea taarifa ya utendaji wa mfuko wetu, hivyo
ninawasihi kama wawekezaji tujadili jinsi ya kuuboresha kupitia fursa zilizopo, tuweke mikakati ya kuongeza
thamani ya uwekezaji wetu ili uwekezaji wetu uwe na manufaa” alisema Mhe. Kikwete.
Aidha, Mhe. Kikwete alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
itaendelea kuthamini mchango wa mifuko ya uwekezaji kama Faida Fund katika
kukuza uchumi, utamaduni wa kuwekeza na kuongeza ustawi wa wananchi.
Kwa upande
mwingine, Waziri Kikwete amewahimiza Watumishi wa Umma kuchangamkia fursa hiyo
ya kujiwekea akiba za kifedha ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya kustaafu. Watumishi wa Umma wanaweza kuwekeza kwa dirisha
la e-Wekeza kupitia makato katika mishahara yao kila mwezi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wawekezaji wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida
Fund) wakati
wa Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka uliofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF jijini Dar es Salaam.
Wawekezaji wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida
Fund) wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza nao kwenye Mkutano
wa Tatu (3) wa Mwaka wa
Mfuko huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF jijini
Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Bw. Sephania
Solomon (wa tatu kutoka kulia) akisubiri kumpokea Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani)
kabla ya Waziri huyo kufungua
Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund)
uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF
jijini Dar es Salaam. Wengine ni Watendaji wa WHI.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye eneo
la ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa
Mfuko wa Uwekezaji wa Faida
(Faida Fund) jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (kushoto) akifurahia jambo wakati akizungumza na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Bw. Sephania
Solomon (kulia) kabla ya Waziri huyo kufungua Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund)
jijini Dar es Salaam.
Watumishi
wa Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakiwa nje ya ukumbi
wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF kwa ajili ya kutoa huduma wakati wa Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa
Mfuko wa Uwekezaji wa Faida
(Faida Fund) uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Wawekezaji wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida
Fund) wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete wakati akizungumza nao kwenye Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa Mfuko huo uliofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF jijini Dar es Salaam.
Watumishi
wa Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakitoa huduma nje ya
ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF wakati wa Mkutano wa tatu (3) wa Mwaka
wa Mfuko wa Uwekezaji wa
Faida (Faida Fund) uliofanyika jijini Dar
es Salaam.
Wawekezaji wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida
Fund) wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete wakati akizungumza nao kwenye Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa Mfuko huo uliofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF jijini Dar es Salaam.
Wawekezaji wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida
Fund) wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete wakati akizungumza nao kwenye Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa Mfuko huo uliofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment