Na. Antonia Mbwambo na Veronica Mwafisi-Morogoro
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ajira mpya 980 zilizotolewa na Serikali kwa
ajili ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) zitaongeza
nguvu katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Mhe. Kikwete amesema hayo wakati akitoa maelezo ya
awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kuzungumza na Viongozi wa TAKUKURU na Wadau
mbalimbali wa Taasisi hiyo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzani, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu
wa Mwaka wa taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Cate mkoani Morogoro.
Amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa kibali cha ajira
hizo na kuwatahadharisha watumishi wa umma kutojihusisha na vitendo vya rushwa.
“Katika kuboresha utendaji kazi wa Utumishi wa Umma nchini hatua kali
zitachukuliwa kwa watumishi watakaojihusisha na vitendo vya rushwa ili kuwa na
utumishi wa umma unaozingatia Taratibu, Kanuni, Sheria na Miongozo,”
amesisitiza.
Mhe. Kikwete ameahidi kuwa, ofisi yake itaendelea
kusimamia taasisi ya TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria na kadri ya maelekezo ya
Mhe. Rais yatakavyotolewa ili kuongeza tija na kutoa haki stahiki kwa wananchi kwa
maendeleo ya Taifa.
Aidha, ameishukuru Serikali kwa uwezeshaji mkubwa
wa mara kwa mara katika taasisi hiyo ikiwemo rasilimaliwatu, fedha ambazo
zimesaidia kujenga majengo mbalimbali ya TAKUKURU na vifaa mbalimbali vya
utendaji kazi.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila amesema ofisi yake inaendelea na utekelezaji wa
shughuli zake kwa mujibu wa Sheria ambapo wamedhamiria kuimarisha kwa vitendo
jitihada za Serikali juu ya mapambano dhidi ya rushwa nchini kwa manufaa ya
wananchi na taifa kwa ujumla.
Aidha, Bw. Chalamila amesema, TAKUKURU inaendelea
na kazi ya kuelimisha umma mijini na vijijini kuhusu masuala ya rushwa na
kufuatilia utekelezaji wa miradi ya Serikali ili kuzuia vitendo vya rushwa kwa
manufaa ya nchi.
Mkutano Mkuu wa mwaka wa Viongozi wa TAKUKURU hufanyika kwa lengo la
kubainisha changamoto
zinazowakabili katika utendaji kazi wao na kutafuta ufumbuzi wa pamoja. Mkutano huu una kaulimbiu ya “Kuzuia
rushwa ni jukumu lako na langu, tutimize wajibu wetu”.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi wa TAKUKURU na wadau
mbalimbali wa Taasisi hiyo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa
Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.
Viongozi wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi wa TAKUKURU na wadau
mbalimbali wa Taasisi hiyo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa
Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba (aliyekaa katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama katika
hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi wa
TAKUKURU uliofanyika leo tarehe 26 Januari, 2026 Mkoani Morogoro. Kulia kwake
ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin
Chalamila
Viongozi
wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete (hayupo pichani) akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano
Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza Kushoto) akiwa tayari kumpokea Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba katika hafla ya
Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi wa TAKUKURU
uliofanyika leo tarehe 26 Januari, 2026 Mkoani Morogoro. Kushoto kwake ni
Katibu Mkuu Ikulu Bw. Mululi Mahendeka
Naibu Mkurugenzi Mkuu
wa TAKUKURU, Bi. Neema Mwakalyelye wa TAKUKURU akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na
Utawala Bora, Bi. Felister Shuli wakati walipokuwa
katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
Mwaka 2025 wa Viongozi wa TAKUKURU uliofanyika Mkoani
Morogoro
Viongozi
wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete (hayupo pichani) akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano
Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.


No comments:
Post a Comment