Na. Mwandishi Wetu-Dodoma
Tarehe
15 Januari, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ametoa rai kwa
Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupitia Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2050 hususani katika eneo la utawala bora kuweka mikakati
ya pamoja ya kuzuia na kupambana na rushwa na kuhakikisha watumishi wao
wanafanya kazi kwa kuzingatia uwazi, usawa na uwajibikaji.
Mhe. Kikwete ametoa rai hiyo Januari 15, 2026 jijini Dodoma wakati
alipotembelea Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuzungumza na watumishi hao na kujitambulisha.
“Mimi na msaidizi wangu Mhe.
Regina Qwaray tunaipongeza Menejimenti na Watumishi kwa kuteleza majukumu yenu
kwa weledi na ufanisi, pia niwahakikishie kuwa sisi tuko tayari kutoa
ushirikiano wa dhati wakati wote ili taasisi yetu iendelee kuaminiwa” alisema
Mhe. Ridhiwani.
Pia, ameitaka TAKUKURU kutangaza
na kusema mafanikio inayoyapata katika utendaji kazi wao na kutoa elimu kwa
umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari hususani mitandao ya kijamii ambayo
kwa sasa ni chombo muhumu cha mawasiliano katika jamii.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray aliongeza
kuwa pamoja na kufika kujitambulisha, pia
wamekwenda kuwakumbusha watumishi hao wajibu wao ili kuweka mshikamano na umoja
katika usimamizi wa miradi ya maendeleo nchini.
“Tumekuja
kujitambulisha ili tupate kufahamiana, hivyo ninaomba tuongeze ari ya kufanya
kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha maono ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo
wananchi” alisema Mhe. Qwaray.
Naye, Bi. Enedy Munthali kwa niaba ya Katibu Mkuu - Ofisi ya Rais
Ikulu amesema kuwa Ofisi yake iko tayari kuendelea kuhakikisha TAKUKURU
inapata rasilimaliwatu na fedha kwa mujibu wa bajeti yao ili kukamilisha
majukumu na miradi kwa wakati.
Pia, Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila amewashukuru mawaziri hao kwa kuitembelea
taasisi hiyo na ameahidi kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa ofisi hiyo kutoa
ushirikiano kwa viongozi hao ili kutekeleza majukumu kwa ufanisi.
Vile vile, TAKUKURU inaendelea
kufanya utafiti ili kubaini mianya ya rushwa na kuzuia na kuhakiksha wananchi
wanapata huduma bora kama Serikali ya
inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyokusudia.
Awali, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi.
Neema Mwakalyelye alimuomba Mhe. Kikwete kufikisha salamu za
shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kuendelea kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara yake ya kikazi iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya
kikazi.
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza
maneno ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuzungumza na Viongozi na Watumishi wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara ya kikazi
iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya
kikazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila wakati Waziri huyo alipotembelea Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara yake ya kikazi iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila akielezea utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo
kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya
Waziri huyo iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Watendaji na
Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakimpigia
makofi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) mara baada ya kuhitimisha
hotuba yake alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
(kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila
(kushoto) alipokuwa akimkabidhi Waziri huyo vitendea kazi vya Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo
jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Maafisa wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi katika taasisi hiyo jijini
Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray
(kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila
(kushoto) alipokuwa akimkabidhi Naibu Waziri huyo vitendea kazi vya Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila (kushoto) akimkabidi vitendea kazi vya Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mwakilishi wa Katibu Mkuu-IKULU,
Bi. Ened Munthali (katikati) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete (wa kwanza kulia) aliyoifanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
akisalimiana na baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati alipowasili katika ofisi hiyo kwa ziara
ya kikazi jijini Dodoma.
Kwaya ya Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ikitoa elimu kupitia nyimbo wakati
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete alipofanya ziara katika ofisi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
(mbele) akiondoka katika ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika ofisi hiyo jijini
Dodoma. Nyuma yake kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray.



No comments:
Post a Comment