Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam
Tarehe 17 Novemba, 2024
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amewataka Waajiri katika Taasisi za Umma kuwapa waajiriwa wapya mafunzo elekezi yanayostahili ili kuondokana na uvunjifu wa maadili na kushtakiana kwa sababu ya kutokuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika Utumishi wa Umma.
Mhe. Sangu ametoa kauli hiyo wakati
wa kikao kazi cha kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika
usimamizi wa Utumishi wa Umma lililofanyika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA) jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Sangu amesema ni vizuri waajiri wakatafuta watu sahihi wa kutoa mafunzo elekezi
kwa waajiriwa wapya badala ya kuchukua watu wa mitaani kwani kwa kufanya hivyo
kunahatarisha ajira za watumishi hao na Utumishi wa Umma kwa ujumla.
“Waajiriwa
wapya wanatakiwa kuelekezwa kwa umakini wa hali ya juu ili wazijue Sheria na Taratibu
za Utumishi wa Umma, hivyo ni vizuri
wakatumika wataalam wanaoweza kufanya kazi hiyo,” Mhe. Sangu amesisitiza.
Aidha,
Mhe. Sangu amesema Rasilimaliwatu ni rasilimali muhimu kuliko rasilimali nyingine
hivyo ni vizuri ikasimamiwa kwa umakini ili kuleta tija kwa taifa.
“Rasilimaliwatu
haitakiwi kuchezewa hata kidogo na ndio maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akiipa kipaumbele katika
kuisimamia kwa kuangalia haki na masilahi ya watumishi,” Mhe. Sangu amesema.
Ameongeza
kuwa mifumo mbalimbali mizuri inayoanzishwa itakuwa haifanyi kazi kikamilifu
kama rasilimaliwatu itachezewa.
Amesema
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iko tayari
kusimamia na kuhakikisha haki na masilahi ya watumishi wa Umma nchini
yanalindwa kama ambavyo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza.
“Ofisi
ya Rais-UTUMISHI itahakikisha watumishi wa umma wanatendewa haki na kulinda
masilahi yao na ndio maana tumeanzisha mifumo mbalimbali ya utekelezaji wa
majukumu.” Mhe. Sangu amesisitiza.
Mhe.
Sangu ameipongeza Menejimenti ya TPA kwa kufanya kazi kwa kuzingatia Taratibu
na Miongozo ambayo imekuwa ikitolewa na Ofisi ya Rais-UTUMISHI.
Amewataka
waajiri wote nchini katika taasisi za umma kuzingatia taratibu na miongozo ya
Utumishi wa Umma ili kuepuka malalamiko ya watumishi na kukwamisha utekelezaji
wa majukumu.
Akimkaribisha
Naibu Waziri Sangu kuzungumza na Menejimenti ya TPA, Mwenyekiti wa Tume ya
Utumishi wa Umma, Mhe.Jaji (Mst) Hamisa Kalombola amesema zoezi la ukaguzi wa
rasilimaliwatu katika utumishi wa umma linafanyika kwa kuzingaria sheria na sio
kwa maamuzi yao binafsi.
“Ukaguzi
wetu umefanyika kwa upande wa Rasilimaliwatu kwani rasilimaliwatu hiyo ndiyo
inayoisaidia Serikali kutekeleza majukumu na kupanga mipango ya maendeleo hivyo
ni muhimu sana kwa taasisi za umma kuzingatia hili.” Mhe. Kalombola ameongeza.
Akitoa
maelezo ya awali, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mbossa ameishukuru Tume
ya Utumishi wa Umma na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora kwa kuwapa ushirikiano na kutoa miongozo
ambayo inawasaidia kuboresha utendaji kazi wa taasisi hiyo hasa katika
eneo la usimamizi wa rasilimaliwatu.
Ukaguzi wa Uzingatiaji wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma ni njia mojawapo ambayo hutumika kupima ni kwa kiwango gani, Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu wanazingatia Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma katika kusimamia Utumishi wa Umma.
Tume ya Utumishi wa
Umma chini ya Kifungu cha 10(1(c) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298,
imepewa mamlaka ya kufuatilia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu katika
usimamizi wa Utumishi wa Umma ikiwemo usimamizi wa masuala ya Rasilimali Watu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza
na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha kuhitimisha
zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mbossa (kulia) akitoa maelezo ya awali kuhusu TPA
wakati wa kikao kazi cha
ofisi hiyo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu kilicholenga kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa
uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es
Salaam.
Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi
wa Bandari Tanzania (TPA) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu wakati
akizungumza nao kwenye kikao kazi cha kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa
uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es
Salaam.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma
Bw. Mathew Kirama akitoa
maelezo kuhusu ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa
Umma uliofanyika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kabla ya kumkaribisha
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Deus Sangu kuzungumza na Menejimenti ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (meza kuu) akiongoza kikao kazi na
Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (RPA) kilicholenga
kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa
Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Timu ya Ukaguzi kutoka Tume ya
Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi cha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu wakati
akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kilicholenga
kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa
Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe.Jaji (Mst) Hamisa Kalombola (kushoto) akitazama nyaraka wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakati wa kikao kazi hicho kilicholenga kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama.
Mkurugenzi wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Mary
Mwakapenda (wa kwanza kulia) akifuatilia kikao kazi cha kuhitimisha zoezi la
ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma kwa Mamlaka
ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria,
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Stanslaus Kagisa akitoa
neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) mara baada
ya Naibu Waziri huyo kufunga kikao kazi na Mamlaka hiyo kilicholenga kuhitimisha
zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment