Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeendelea kutoa mafunzo elekezi kwa watumishi wa ofisi yake kwa lengo la kuboresha utendaji kazi ili kuwawezesha watumishi hao kutoa huduma bora kwa wananchi na wadau mbalimbali wa Serikali.
Akiwasilisha mada
kuhusu Huduma kwa Mteja, Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji
Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Emmanuel Luvanda amesema malengo ya Utumishi wa Umma ni kuwahudumia wananchi kwa kiwango cha hali
ya juu, hivyo kila mtumishi ni vizuri akawajibika kikamilifu ili kufikia
malengo hayo.
Bw. Luvanda ameongeza
kuwa, kwa kuendelea kuwajibika kwa wananchi kwa kutoa huduma bora kwao
kunawafanya wawe na imani kubwa na Serikali yao.
Aidha, Bw. Luvanda
amewashauri watumishi wa Ofisi hiyo kutumia changamoto mbalimbali kama fursa ya
kujifunza na kuona namna ya kutatua changamoto hizo na kuleta maboresho yenye
ufanisi mkubwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bw. Musa Magufuli ametoa wito kwa watumishi wa ofisi hiyo kuwahudumia wadau wote wanaohitaji huduma katika ofisi hiyo kwa kuzingatia misingi ya huduma bora ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi pamoja na kujenga taswira nzuri ya ofisi.
Mafunzo hayo elekezi
ni utaratibu uliowekwa na Ofisi hiyo kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu masuala
mbalimbali ya Utumishi wa Umma ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao
ipasavyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli (aliyenyoosha
mkono) akizungumza baada ya kumalizika mafunzo
ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika
katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya
kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika
katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Wakurugenzi
wasaidizi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI
na Utawala Bora wakimsikiliza Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka
ofisi hiyo Bw. Emmanuel Luvanda (hayupo pichani)
wakati akifanya wasilisho
kuhusu Huduma kwa Mteja walipokuwa kwenye mafunzo ya kuwajengea
uwezo katika masuala
ya utendaji kazi.
Afisa Utumishi
Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Bw. Emmanuel Luvanda (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu Huduma
kwa Mteja wakati wa
mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala
Bora yaliyofanyika
katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya
kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika
katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mtumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala
Bora, Bi. Zena Makaye
(aliyesimama) akichangia hoja wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo
watumishi hao katika utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji
wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mtumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala
Bora, Bw. Baraka Kilagu
(aliyesimama) akiwasilisha hoja wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo
watumishi hao katika utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji
wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment