Saturday, November 16, 2024

NAIBU WAZIRI SANGU: MKOA WA KIGOMA SIO SEHEMU YA KUPATIA AJIRA NA KUHAMA


 

 

Na Lusungu Helela- Kigoma


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amesema Kigoma sio Mkoa wa kupatia cheki namba  (ajira) na  kuhama kwa visingizio vya kuifuata familia au kwa  sababu za ugonjwa huku akiwataka watumishi hao kuachana na dhana  ya kuwa Mkoa ni wa pembezoni na hauna fursa za kiuchumi.


Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na     Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, ikiwa ni kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili  Watumishi hao.


Amesema yeye kwa kushirikiana na Waziri wake Mhe. George Simbachawene wamelazimika kuweka utaratibu wa kufanya Klikini hiyo katika Mikoa mbalimbali nchini baada ya kuona Watumishi wengi wanalazimika kusafiri hadi jijini Dodoma kwa ajili ya changamoto walizonazo za kiutumishi ambazo zingeweza kutatuliwa papo kwa papo na Maafisa Utumishi wao.


Mhe.Sangu amesema kuna dhana imejengeka kuwa Mikoa ya Magharibi ikiwemo Katavi, Kigoma na Rukwa kuwa ni Mikoa ya adhabu kwa watumishi ambao wamepangiwa kufanya kazi katika maeneo hayo, jambo ambalo sio kweli hii inatokana na   uboreshaji mkubwa  wa miundombinu uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita.


‘’Kumekuwa na wimbi kubwa la Watumishi wa Umma mara tu baada ya kupata ajira huja kuripoti Mkoani Kigoma  huanza taratibu za kuomba uhamisho, jambo hili sio sawa kwani wananchi wa Kigoma nao wanahitaji huduma bora kama wananchi  wa Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza.’’ Amesisitiza Mhe. Sangu

 

Amesema Mtumishi wa Umma atalazimika kuhama katika Mkoa huo endapo atakuwa amekaa miaka mitatu na kuendelea na pia kama atakuwa amepata Mtumishi mwenzake wa kubadilishana nae.

 

Hata hivyo, Mhe. Sangu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka mitatu ametoa zaidi ya Trioni 11 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ikiwemo barabara na huduma mbalimbali ikiwemo za afya pamoja na elimu katika Mkoa huo.

 

Amesema kutokana na uboreshaji wa miundombinu hiyo  kwa sasa Kigoma haina tofauti na Dodoma na Arusha kwani ina kila aina ya fursa pamoja na  miundombinu mizuri

 

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Kirumbe Ng’enda  amesema Kigoma inahitaji watumishi wachache lakini wenye utayari wa kufanya kazi katika Mkoa huo na sio wale walioletwa baada ya kufanya vibaya katika mikoa mingine.

Awali, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Mbwilo Elisante  amesema Mkoa wa Kigoma unakabiliwa na uhaba mkubwa wa Watumishi kwani   Watumishi wengi huhamishwa bila ya kuletwa mbadala.

 

 

 

 




 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akizungumza leo na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, ikiwa ni kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi  changamoto zinazowakabili




 Sehemu ya Watumishi wa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu wakimskiliza katika Kikao kazi kilichofanyika kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi







Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe.  Thobias Andengenye mara baada ya mazungumzo ofisini kwake leo akiwa kwenye ziara ya  kuzungumza na  Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, ikiwa ni kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi  changamoto zinazowakabili

 

 



 

Meneja wa TRA WA  Mkoa wa Kigoma, Deogratius Shuma akitoa neno la shukrani  kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu wakati wa kikao hicho kilichofanyika leo Mkoani  Kigoma



 


 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akizungumza leo na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, ikiwa ni kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi  changamoto zinazowakabili

    

Kaimu Meneja wa Kanda ya Magharibi, Stanley Ganzel akiuliza swali 

mbele ya    Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu kabla ya  kuzungumza  na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, ikiwa ni kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi  changamoto zinazowakabili

 

No comments:

Post a Comment