Na. Lusungu Helela
Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw.
Juma Mkomi amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Japan ( JICA), Bw. Ara Hitoshi kuhusu kuimarisha
ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala
Bora.
Kikao hicho
kimefanyika leo Ijumaa Novemba 8, 2024 katika Ofisi zilizopo Mji wa
Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Miongoni mwa masuala
waliyojadili ni pamoja na kutoa fursa za mafunzo kwa watumishi pamoja na
maombi ya vibali vya ajira kwa raia wa kutoka Japan wanaokuja
kufanya kazi nchini katika miradi ya Serikali katika Utumishi wa Umma
ambapo fursa hiyo huwasaidia Wazawa kubaki na ujuzi unaoweza
kutumika hata baada ya miradi ya maendeleo kukamilika
Aidha, viongozi hao wamepongeza juhudi za ushirikiano wa nchi hizo mbili unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Japan, Mhe. Shigeru Ishiba.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI
Bw. Juma Mkomi akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo la Japan ( JICA), Bw. Ara Hitoshi mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha
ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala
Bora.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI
Bw. Juma Mkomi akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo la Japan ( JICA), Bw. Ara Hitoshi mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha
ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala
Bora.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Juma Mkomi akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan ( JICA), Bw. Ara Hitoshi mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Juma Mkomi akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan ( JICA), Bw. Ara Hitoshi kuhusu kuimarisha ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora.
No comments:
Post a Comment