Monday, November 4, 2024

SERIKALI YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUWA NA MIENENDO INAYOKUBALIKA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Na Lusungu Helela-Dodoma

Serikali imewataka Watumishi wa Umma nchini  kuwa na mienendo inayokubalika  katika  utumishi wa umma kwa kutumia  madaraka waliyopewa kwa usahihi ili kuepukana  na mgongano wa maslahi  wanapokuwa kazini.

 Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Usimamizi wa Maadili Bi. Janet Mishinga  amesema hayo leo Jumatatu Novemba  4, 2024 wakati akitoa mafunzo ya Kanuni ya Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa  Watumishi wa  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Katika Ofisi zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba  jijini Dodoma ambapo amesema kanuni hizo ni  muhimu kwa Watumishi wote kuzielewa.

Amesema endapo  Watumishi wa Umma watazielewa ipasavyo kanuni hizo wataweza  kutumia rasilimali  za Umma kwa manufaa ya Umma huku akitolea mifano ya rasilimali hizo ikiwa ni pamoja na   mitambo, simu  kompyuta  na  majengo 

Aidha, Bi. Mishinga amewataka Watumishi wa Umma  kuwatendea haki  wateja wote  bila kujali hadhi, jinsi, dini, umri, kabila au itikadi za kisiasa.

‘’ Tunatakiwa kutoa huduma bora  kwa wateja wetu kwa kuzingatia Sheria,  Taratibu na Kanuni na kamwe tujiepushe na upendeleo wa aina yeyote ile’’ amesisitiza Bi. Mishinga

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Elibariki Kahungya  amesema mafunzo hayo ni muendelezo ambapo kila jumatatu ya wiki yatakuwa yakifanyika  lengo likiwa ni kujengeana uwezo kwa watumishi wote 

" Mafunzo haya ni muhimu kwa watumishi wote,  hivyo naomba tuzingatie muda ili yaweze kuanza kulingana na muda ambao tumejipangia ‘’ amesisitiza Bw. Kahungya

          Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Usimamizi wa Maadili Bi. Janet Mishinga akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

     Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Usimamizi wa Maadili Bi. Janet Mishinga  (hayupo pichani) wakati akizungumza nao wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi wasaidizi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Usimamizi wa Maadili Bi. Janet Mishinga (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

     Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Usimamizi wa Maadili Bi. Janet Mishinga   (hayupo pichani) wakati akizungumza nao wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

     Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Usimamizi wa Maadili Bi. Janet Mishinga    (hayupo pichani) wakati akizungumza nao wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment