NAIBU WAZIRI SANGU: e-GA NI TAASISI NYETI KWA USALAMA WA TAIFA
Na.
Lusungu Helela
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu amesema
Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ni Taasisi nyeti kwa ajili ya
usalama wa nchi kwani kwani hakuna Mfumo wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) uliosanifiwa unaoweza kutumika nchini katika Wizara,
Taasisi au Idara ya Serikali bila kuridhiwa na e-GA
Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo
leo jijini Dodoma wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria katika kikao cha Kamati hiyo na Watendaji
wa e-GA na Taasisi ya Uongozi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya
utendaji kazi wa Taasisi hizo ambapo amesema
tangu kuanzishwa kwake e-GA imeleta mageuzi makubwa huku akitaja mifumo
mingi inayotumika kwa sasa Serikalini imebuniwa na kusanifiwa
na e-GA
Amesema ujio wa e-GA
umeisaidia kupunguza gharama kubwa kwa Serikali ukilinganisha na hapo
awali ambapo mifumo mingi iliyokuwa ikitumika kwenye Taasisi za Serikali
ilikuwa ni ya kutoka nje huku akitolea mfano mfumo wa manunuzi wa
TANEPS ulikuwa ukimlazimisha mtumiaji endapo kama anataka kufanya marekebisho
ni lazima awasiliane na watengenezaji wa mfumo huo ambao ni
Wagiriki
" Kama nchi kulikuwa
hakuna usiri wa taarifa zetu, Wasanifishaji mifumo ya TEHAMA ambao ni wa kutoka
Mataifa ya nje ndo walikuwa wenye ‘serve’ za taarifa zetu amesisitiza Mhe.Sangu
Amesema hapo awali Taasisi nyingi za Serikali zilikuwa
zikitumia mifumo hiyo ya kutoka nje bila kuidhinishwa na e-GA ambapo ilikuwa ni rahisi kuhujumu kwa lengo la kujinufaisha
kwa kushirikiana na watu wa kutoka nje ila kwa sasa hilo jambo haliwezekani
kutokana na uwepo wa e-GA
'" Upo ushahidi kabisa
kwamba e-GA imesaidia kuboresha utendaji kazi, imeimarisha utawala bora, kupunguza
vitendo vya rushwa ambavyo vingeweza kujitokeza, kuimarisha makusanyo na
kudhibiti matumizi ya maduhuli ya serikali” Mhe. Sangu amesisitiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria
Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ameipongeza e-GA kwa kazi kubwa inayoendelea
kuifanya huku akiitaka kjiimarisha zaidi kwenye eneo la ubunifu ili kuendana na
kasi ya mabadiliko ya teknolojia yanayotokea dunia kote
Hata hivyo Mwenyekiti huyo
ameitaka e-GA kusanifu mifumo itakayosaidia kupunguza matatizo katika jamii
ikiwemo upotevu mkubwa wa maji unaotokea katika maeneo mbalimbali nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Watendaji wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hizo
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi , Bw. Kadari Singo,akiwasilisha hoja kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi
Sehemu ya Watendaji wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hizo
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi
Mtendaji Mkuu wa e-GA, Mhandisi Benedict Ndomba,akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao kazi cha kamati
hiyo na Watendaji wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya
Uongozi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi
hizo
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Hussein Amar akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo
pamoja na watendaji wa Mamlaka ya
Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji
kazi wa Taasisi hizo
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao kazi cha kamati
hiyo na Watendaji wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya
Uongozi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi
hizo
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Oscar Kikoyo akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo
pamoja na watendaji wa Mamlaka ya
Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji
kazi wa Taasisi hizo
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Abdullah Ali Mwinyi akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hizo
No comments:
Post a Comment