Saturday, November 16, 2024

WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA WAAJIRI KUZINGATIA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI ILI KULINDA NGUVU KAZI YA TAIFA

 Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam

Tarehe 16 Novemba, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametoa rai kwa Waajiri katika Taasisi zote za Serikali kuhakikisha zinatekeleza Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi Na. 5 ya mwaka 2003 ili kulinda nguvu kazi ya Taifa na kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi.

Mhe. Simbawewene ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Novemba, 2024 alipotembelea Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) jijini Dar es Salaam kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa utumishi wa umma.

Mhe. Simbachawene amesema Sheria hiyo ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi inaelekeza maeneo yote ya kazi nchini kuwa na Mifumo madhubuti ya kuwakinga Wafanyakazi dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Ameongeza kuwa, kwa kutambua umuhimu wa usalama na afya mahali pa kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ilitunga Kanuni ya 105 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2022 inayoelekeza Waajiri kuchukua tahadhari zote dhidi ya ajali na magonjwa mahali pa kazi.

Ameipongeza Menejimenti ya OSHA kwa kuendelea kuisimamia Sheria hiyo na kuhakikisha kuwa Waajiri wanasimamia kikamilifu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi ili kuwakinga watumishi wa Umma dhidi ya magonjwa, ajali na hata vifo.

Amesema kwa mujibu wa Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 1998, Tume ya Utumishi wa Umma iliundwa ili kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unakuwa mmoja na watumishi wa umma wanakuwa na Taratibu za usimamizi wa utumishi wao unaofanana. Hivyo, Ukaguzi wa Uzingatiaji wa Sheria katika Usimamizi  wa Utumishi wa Umma ni njia mojawapo ambayo hutumika kupima ni kwa kiwango gani, Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu wanazingatia Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma katika kusimamia Utumishi wa Umma. 

Tume ya Utumishi wa Umma chini ya Kifungu cha 10(1(c) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298, imepewa mamlaka ya kufuatilia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu katika usimamizi wa Utumishi wa Umma ikiwemo usimamizi wa masuala ya Rasilimali Watu.

Akimkaribisha Waziri Simbachawene kuzungumza na Menejimenti ya OSHA, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Jaji (Mst) Hamisa Kalombola amesema Tume imejiwekea utaratibu wa Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambao ndio wasimamizi wa Tume hiyo kushiriki katika kuhitimisha zoezi la ukaguzi uliofanyika kwa taasisi ili kushuhudia namna zoezi lilivyofanyika.

Akitoa maelezo ya awali, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda amesema ili nchi iendee inahitaji nguvu kazi yenye afya, hivyo jukumu lao ni kuhakikisha mifumo  ya kulinda afya za watumishi inawekwa katika taasisi za umma na binafsi ili kuzuia magonjwa yanayotokana na kazi hayaathiri utendaji kazi wa watumishi

Kwa upande wake Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama ameyataja maeneo ambayo Tume imeyakagua kuwa ni ajira mpya, upandishaji vyeo, mafunzo na maendeleo ya watumishi, nidhamu, likizo ya kustaafu na uzazi, uzingatiaji wa maadili, ushughulikiaji wa mrejesho, usimamizi wa taratibu za ofisi ikiwemo utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka, anuai za jamii, mfumo jumuishi wa taarifa za kiutumishi na mishahara, fidia ya ajali pamoja na magonjwa yanayotokana na kazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.


Menejimenti ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye kikao kazi cha kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Jaji (Mst) Hamisa Kalombola (aliyesimama) akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Menejimenti ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakati Waziri huyo alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama akitoa maelezo kuhusu ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma uliofanyika kwenye ofisi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.


Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi.  Khadija Mwenda (aliyesimama) akitoa maelezo ya awali kuhusu OSHA wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.


Mkaguzi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma, Bi. Kombe Shayo (aliyekaa kulia) akitoa maelezo ya namna Mfumo wa Ukaguzi unavyofanya kazi wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipotembelea ofisi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa lengo la kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe.Jaji (Mst) Hamisa Kalombola (wa pili kutoka kulia) na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama (wa kwanza kulia), wengine ni Viongozi na Watendaji wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA).


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) akipokea vitendea kazi vya ofisi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi.  Khadija Mwenda (kushoto) mara baada ya Waziri huyo kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment