Na. Veronica Mwafisi-Arusha
Tarehe 04 Novemba, 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewaasa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) kuwa wabunifu katika kusimamia vizuri rasilimaliwatu ili kuondokana na changamoto mbalimbali za watumishi wa umma na kukuza sekta hiyo kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo makubwa katika Bara la Afrika.
Mhe.
Simbachawene ametoa kauli hiyo leo tarehe 04 Novemba, 2024 alipokuwa
akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kufungua Mkutano wa 9 wa Mtandao
wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika
(APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
“Mkutano huu wa Mtandao wa
Mameneja Rasilimaliwatu umefanyika katika kipindi ambacho dunia ina changamoto
mbalimbali hivyo niwaase mtumie fursa ya mijadala mtakayoiendesha na mawazo
mtakayoyatoa kupitia maazimio na mapendekezo yalete mtazamo chanya katika kutoa
majawabu yatakayosaidia kukuza sekta ya umma kiuchumi na kijamii.” Amesema Mhe.
Simbachawene
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, kupitia kaulimbiu
ya mkutano huo inaonyesha ni kwa namna gani rasilimaliwatu katika utumishi wa
umma ni nyenzo muhimu na ya thamani kubwa katika kila nchi ambapo Serikali
huitumia kuwafikia wananchi wake katika kutoa huduma za kijamii na kiuchumi ili
kukuza ustawi wa jamii husika.
Aidha, Mhe. Simbachawene amewapongeza wawezeshaji wa Mkutano huo kwa mada mbalimbali walizozitoa kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo ambazo kwa asilimia kubwa zitasaidia kuleta mabadiliko katika utendaji kazi kupitia rasilimaliwatu zilizopo katika Bara la Afrika.
Kwa upande wake, Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu
katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi, amesema kuwa katika mkutano huo wa 9 wajumbe watapata fursa ya kubadilishana
uzoefu na utaalamu kwa lengo la kuwezesha nchi za Bara la Afrika kupiga hatua
za kimaendeleo kwa kutumia mbinu za kisasa.
“Mtandao
huu umeanzishwa kwa lengo la kujenga uwezo wa rasilimaliwatu yenye matokeo chanya
katika kuhudumia wananchi Barani Afrika hivyo kupitia Mkutano huu tutapata fursa
ya kubadilishana uzoefu na utaalamu ili kuzisaidia nchi zetu kujikwamua
kiuchumi na kuleta maendeleo kwa mataifa.” Bw. Daudi amesema.
Mkutano huo wa
Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) uliofunguliwa
na Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan unatarajiwa kufanyika
kwa muda wa siku nne kuanzia leo tarehe
4 hadi 7 Novemba, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini
Arusha.
Kaulimbiu ya Mkutano
huo ni ‘Utawala Stahimilivu na Ubunifu: Kukuza Sekta
ya Umma ijayo kupitia Uongozi wa Rasilimaliwatu’.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
kufungua Mkutano wa 9 wa
Mtandao wa Mameneja
Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Baadhi ya Washiriki wa
Mkutano wa 9 wa Mtandao
wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) wakimsikiliza Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa
Mkutano huo unaofanyika
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika
Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akielezea
malengo ya Mkutano wa 9 wa
Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu
katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
(Wa kwanza kushoto) akimsikiliza mtumishi
wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Vincent Ngure
wakati akielezea mifumo ya kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya utumishi wa
umma wakati wa Mkutano wa 9 wa Mtandao
wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika
(APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya
washiriki wa mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya
Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi
Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said akisalimiana na Makamu wa Rais wa Mtandao wa
Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) Bw. James
Wasagami (Wa kwanza kulia) wakati alipowasili kushiriki kwenye
ufunguzi
wa Mkutano wa 9 wa mtandao huo unaofanyika
katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Wa pili kutoka kulia ni Rais wa
Mtandao huo (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi na wa
tatu kutoka kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
Bw. Juma Mkomi.
Mtumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Bi. Theresia Ngassa (kushoto) akigawa kablasha na kitambulisho
kwa mmoja wa washiriki wa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu
katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na Prof. Patrice Lumumba ambaye ni Msemaji Mkuu wa Mkutano wa 9 wa
Mtandao wa Mameneja
Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Wa
kwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na
Utawala Bora Zanzibar, Mhe.
Haroun Ali Suleiman.
Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika picha ya pamoja tayari kwa kutoa huduma kwa washiriki wa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika
(APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI
na Utawala Bora wakifuatilia usajili wa mshiriki wa Mkutano
9 wa
Mtandao wa Mameneja
Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika
Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI
na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli wakati wa Mkutano wa
9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika
(APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
No comments:
Post a Comment