Wednesday, November 20, 2024

NAIBU WAZIRI SANGU ASHANGAZWA NA IDADI NDOGO YA WAOMBAJI AJIRA KATIKA MIKOA YA KIGOMA, LINDI, MTWARA NA KATAVI

 

Na Lusungu Helela- Katavi 

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameonesha  kushangazwa na idadi ndogo ya waombaji wa nafasi za kazi  kada ya afya waliokuwa wameomba katika Mikoa ya Kigoma,  Katavi, Lindi na Mtwara huku Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma ikiwa na idadi kubwa ya waombaji ukilinganisha na  uhitaji.

 

Hatua hii inakuja kufuatia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuweka utaratibu wa kuomba ajira katika mkoa husika kulingana na uhitaji ambapo Mwezi Juni mwaka huu ilitangaza jumla ya nafasi za kazi 9483 za kada ya afya ambapo kila muombaji alilazimika kuomba ajira katika mkoa ambao atafanya kazi endapo atafanikiwa kupita kwenye usaili.

 

Amesema  licha ya tatizo kubwa la ajira linalowakumba vijana wengi  lakini bado waombaji hao  wanataka kuanza  kufanya  kazi katika Majiji makubwa jambo ambalo ni gumu 

 

Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na     Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa  kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili  Watumishi hao.

 

Akitolea mfano Mkoa wa Kigoma  mahitaji halisi ya waliotakiwa kuajiriwa katika kada ya afya ilikuwa ni 400 lakini waombaji wa nafasi hizo walikuwa hawazidi 200 huku Mikoa ya Lindi, Mtwara na Katavi nako idadi ni ndogo ukilinganisha na uhitaji.

 

 

Kufuatia hatua hiyo Mhe.Sangu ametoa wito kwa wazazi kuwashawishi watoto wao kuomba ajira pindi zinapotangazwa  katika mikoa hiyo kwani uwezekano wa kupata ni mkubwa ukilinganisha na mikoa kama vile Arusha na Dodoma ambako ushindani ni mkubwa.

 

Hata hivyo Mhe.Sangu amewaonya wale watakaoomba kazi katika mikoa hiyo halafu wakapangiwa,  Serikali haitawavumilia endapo wataanza kuomba uhamisho kabla ya kufanya kazi kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

 

Vilevile Mhe.Sangu amesema mikoa hiyo haina tofauti na Mwanza, Dar es Salaam, Dodoma na Arusha kwani ina fursa za kiuchumi pamoja na miundombinu iliyoboreshwa huku   akiwataka wenye uhitaji wa ajira kuchangamkia ajira zinapotangazwa kwenye mikoa hiyo.

 

Awali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Abert Msovela  amesema licha ya uwepo wa fursa za kiuchumi katika mkoa huo lakini bado idadi ya Watumishi wa Umma wanaotuma maombi ya kutaka kuhama ni mengi.

 

Ametumia fursa hiyo kuwaasa Watumishi kubadili kasumba hiyo kwani  Mkoa wa Katavi kwa sasa ni Mkoa wa kutimiza ndoto za kila Mtumishi mwenye kutaka kujikwamua kiuchumi kutokana na uwepo wa fursa lukuki za kiuchumi ikiwemo ardhi yenye rutuba.









Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na     Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa  kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili  Watumishi hao.


 



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Katavi  wakati akiwasili kwa ajili ya kuzungumza na     Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa  kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili  Watumishi hao.




Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi,  Mhe. Jamila Yusuph kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangua kuzungumza na     Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa  kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili  Watumishi hao.



 Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangua kuzungumza na     Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa  kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili  Watumishi hao.







.

 Baadhi ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakizungumza mbele ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangua kabla ya kuanza  kuzungumza na     Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa  kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili  Watumishi hao 



Miongoni mwa  Watumishi wa Halmashauri ya  Wilaya ya Mpanda akizungumza mbele ya   Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangua kabla ya kuanza  kuzungumza nao  ikiwa ni muendelezo wa  kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili  Watumishi hao.




No comments:

Post a Comment