Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kulia) akizungumza jambo na Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi. Katikati ni Makamu wa Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) Bw. James Wasagami.
Mawaziri na Viongozi mbalimbali kutoka Bara la Afrika
(meza kuu) wakitoa uzoefu wao kuhusu usimamizi wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma wakati wa Mkutano wa 9 wa
Mwaka wa Mtandao wa Mameneja
Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika
(APS-HRMnet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Bw. Juma Mkomi (Wa kwanza kulia) akifuatilia Mkutano wa 9 wa Mwaka wa
Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Kulia kwake ni Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Bw. Omar
Gora.
Mawaziri na Viongozi mbalimbali kutoka Bara la Afrika
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa uzoefu wao kuhusu usimamizi
wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakati wa Mkutano wa 9 wa
Mwaka wa Mtandao wa Mameneja
Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa Arusha (AICC).
Mtumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Bw. Vincent Ngure akielezea mifumo ya kuwezesha
utekelezaji wa majukumu ya utumishi wa umma kwa baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 9 wa
Mwaka wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika
(APS-HRMnet) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Baadhi ya wajumbe wa sekretarieti ya maandalizi ya
Mkutano wa 9 wa
Mwaka wa Mtandao wa Mameneja
Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) wakiwa katika picha ya
pamoja katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
No comments:
Post a Comment