Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 26 Novemba, 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewasisitiza Watumishi wa Umma na Watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura kujitokeza kufanya uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika kesho tarehe 27 Novemba, 2024 Tanzania Bara.
Mhe. Simbachawene ametoa rai hiyo leo akiwa Ofisini kwake katika Mji wa Serikali, Mtumba, Jijini Dodoma.
Mhe.
Simbachawene amesema, zoezi la kesho ni la kihistoria katika nchi yetu hivyo kila
Mtanzania mwenye sifa wakiwemo Watumishi wa Umma wote ni muhimu wakashiriki
katika kuwachagua Wenyeviti wa Serikali za Mitaa,
Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
“Kwa kuwa zoezi hili ni la kikatiba, nikiwa ndiye Waziri mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ninatoa rai kwa Watumishi wote wa Umma na wananchi wote waliojiandikisha kujitokeza kupiga kura ili kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya taifa letu.” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Ameongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza siku ya Jumatano tarehe 27 Novemba,
2024 kuwa ni siku ya mapumziko ili kutoa nafasi kwa watumishi wote kwenda
kupiga kura. Hivyo, Watumishi wa umma kutokushiriki kwenye mambo muhimu ya
kikatiba ni upungufu katika kutekeleza majukumu ya kiutumishi, hivyo amewasisitiza
kwenda kupiga kura bila kupuuza.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akisisitiza Watumishi wa Umma na Watanzania kushiriki Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
No comments:
Post a Comment