Na. Veronica Mwafisi-Arusha
Tarehe 07 Novemba, 2024
Mameneja
Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) wamemuunga mkono Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutangaza
sekta ya utalii katika nchi zao baada ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro
ambayo ni moja ya vivutio maarufu duniani.
Akiongoza
ziara ya Mameneja hao baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa 9 wa Rasilimaliwatu
katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet), Rais wa Mtandao huo ambaye pia ni
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amesema waliona ni vema Mameneja hao kutoka nchi mbalimbali wakatembelea
Hifadhi hiyo ili kuunga mkono jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
ambaye amekuwa mstari wa mbele kutangaza sekta ya utalii ili kukuza uchumi wa
Tanzania.
“Tuliona si jambo jema viongozi
hawa wa Rasilimaliwatu wakarudi nchini kwao bila kufanya utalii, hivyo tukaamua
kuratibu safari ya kwenda Ngorongoro kwani kwa kufanya hivyo tunaamini
watatusaidia kwenda kutangaza utalii wa Tanzani katika nchini zao na kukuza
pato la taifa.” Bw. Daudi amesisitiza.
Bw. Daudi amesema Mameneja hao wameweza kuona
vivutio mbalimbali katika Hifadhi hiyo ya Ngorongoro ikiwemo wanyama, mandhari ya
kuvutia pamoja na kujifunza masuala mbalimbali.
Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja
Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) uliofunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umehitimishwa rasmi baada ya kufanyika kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe
4 hadi 7 Novemba, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini
Arusha.
Mkutano huo ulibebwa na Kaulimbiu isemayo ‘Utawala Stahimilivu na Ubunifu: Kukuza Sekta ya Umma
ijayo kupitia Uongozi wa Rasilimaliwatu’.
Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika
Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akizungumza wakati Wajumbe wa Mkutano wa 9 wa
Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu
katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya
Ngorongoro.
Baadhi ya Watumishi
wa Ofisi ya Rais, Meneimenti ya Utumishi wa Umma na Utawaloa Bora wakifurahia kufika
Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro baada ya kuhitimishwa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya
Umma Afrika (APS-HRMnet) uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika
Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (Wa kwanza kulia) akifurahia
jambo na baadhi ya Viongozi kutoka Barani Afrika walipotembelea Hifadhi ya
Taifa ya Ngorongoro mara baada ya kuhitimishwa Mkutano wa 9 wa
APS-HRMnet uliofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Mjumbe wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) kutoka nchini Kenya akielezea namna alivyofurahia kuona wanyama na vivutio mbalimbali vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro wakati wajumbe wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro mara baada ya kuhitimishwa Mkutano wa 9 wa APS-HRMnet uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Rais wa Mtandao wa Mameneja wa
Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) ambaye pia ni Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (kushoto)
akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Mtandao wa Mameneja
Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) Bw. James Wasagami walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro mara baada ya kuhitimishwa Mkutano wa 9 wa
APS-HRMnet
uliofanyika
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
No comments:
Post a Comment