Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 20 Novemba, 2024
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amewahimiza Viongozi katika Utumishi wa Umma kuzingatia uadilifu wakati wa ujazaji wa fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa masilahi mapana ya taifa.
Katibu Mkuu Mkomi ameyasema hayo leo
tarehe 13 Novemba, 2024 wakati wa mafunzo ya ujazaji wa fomu za Tamko la
Rasilimali na Madeni kwa njia ya kielektroniki yaliyotolewa na Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Menejimenti na Wakurugenzi Wasaidizi wa Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika Ofisi ya Mtumba jijini
Dodoma.
“Nilitoa maelekezo ya kupewa
mafunzo, niwapongeze waratibu wa Ofisi yangu na Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma kwa kuitikia wito wa kuja kutupatia mafunzo haya muhimu ya
ujazaji wa fomu hizi kwa njia ya kielektroniki,” Bw. Mkomi amesisitiza.
Amesema mafunzo haya ni muhimu
kwasababu viongozi walizoea kujaza kwa njia ya karatasi, hivyo ni vema
wakafundishwa namna ya kujaza ili waweze kujaza kwa ufasaha.
“Mafunzo haya ni muhimu na yenye
tija, tuwasikilize kwa makini wakufunzi wetu ili tuweze kujaza kwa ufasaha na
kuwa wakweli kwani tukidanganya mifumo itatuumbua kwa kuwa sasa mifumo
mbalimbali inasomana,” Bw. Mkomi amesisitiza.
Ameipongeza Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma kwa kuanzisha ujazaji wa fomu za matamko kwa njia ya kieletroniki
na kuwasisitiza kutoa uelewa kwa taasisi za Serikali ili wasipate changamoto
katika ujazaji.
“Kwa kuwa mfumo huu wa ujazaji ni
mpya, basi ingekuwa ni vizuri mkajipanga kwa kushirikiana na Idara yangu ya
Uendelezaji Maadili ili kutoa elimu ya namna ya kujaza.” Katibu Mkuu Mkomi
ameongeza.
Awali Katibu wa Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Waziri Kipacha amesema ujazaji wa Tamko la
Rasilimali na Madeni ni takwa la kisheria kwa mujibu wa Kifungu cha 9 cha
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Ameongea kuwa, kwa Viongozi wote
ambao wametajwa kwenye Fungu la 4 la Sheria ya Maadili wa Viongozi wa Umma
pamoja na Marekebisho ya Orodha ya Viongozi ambayo yalifanywa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tangazo la Serikali Namba 856 lililoorodhesha
viongozi wote wa umma wanaowajibika chini ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma,
wanawajibika kutoa tamko kuhusu rasilimali na madeni yao.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza
wakati
wa mafunzo ya ujazaji wa fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya
kielektroniki yaliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa
Menejimenti na Wakurugenzi Wasaidizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora
katika Ofisi ya
Mtumba jijini Dodoma.
Sehemu ya Menejimenti na Wakurugenzi Wasaidizi
wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi alipokuwa akizungumza nao kabla ya kuanza kwa mafunzo
ya ujazaji wa fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya kielektroniki
yaliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Menejimenti
hiyo katika
Ofisi ya Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Usimamizi wa Maadili,
Bi. Leila Mavika akielezea malengo
ya mafunzo ya
ujazaji wa fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya kielektroniki
yaliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Menejimenti na
Wakurugenzi Wasaidizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora
katika Ofisi ya Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kulia) akifuatilia mafunzo ya ujazaji wa fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni
kwa njia ya kielektroniki yaliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma kwa Menejimenti na Wakurugenzi Wasaidizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora
katika Ofisi ya Mtumba jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa
ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi.
Baadhi ya Menejimenti
na Wakurugenzi Wasaidizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora wakifuatilia mafunzo
ya ujazaji wa fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya kielektroniki
yaliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Menejimenti hiyo katika
Ofisi ya Mtumba jijini Dodoma.
Katibu wa Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma, Bw. Waziri Kipacha akifafanua
jambo kwa Menejimenti
na Wakurugenzi Wasaidizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora wakati wa mafunzo ya ujazaji wa fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni
kwa njia ya kielektroniki yaliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma kwa Menejimenti hiyo katika Ofisi iliyopo Mtumba jijini Dodoma.
Sehemu ya Menejimenti na Wakurugenzi Wasaidizi
wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia
mafunzo ya ujazaji wa fomu za Tamko
la Rasilimali na Madeni kwa njia ya kielektroniki yaliyotolewa na Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Menejimenti
hiyo
katika
Ofisi ya Mtumba jijini Dodoma.
Afisa
Tehama, kutoka Ofisi ya Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Musa Mwakasambala akitoa mafunzo kwa Menejimenti na Wakurugenzi Wasaidizi
wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora namna ya ujazaji wa fomu za Tamko la
Rasilimali na Madeni kwa njia ya kielektroniki yaliyotolewa na Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Menejimenti hiyo jijini Dodoma.
Sehemu ya Menejimenti na Wakurugenzi Wasaidizi
wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi alipokuwa akizungumza nao kabla ya kuanza kwa mafunzo
ya ujazaji wa fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya kielektroniki
yaliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Menejimenti
hiyo katika
Ofisi ya Mtumba jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment