“Tambueni kuwa Utumishi wa Umma ni kazi ya Mungu, fanyeni uamuzi kwa kuzingatia sheria za nchi na za kimataifa na msiwe na jaziba, visasi wala upendeleo ili kulinda maslahi ya Taifa”
Wito huo umetolewa Novemba18, 2024 na Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Taaluma Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.
Salim Ahmed Salim, Dkt. Juma Kanuwa wakati akifanya
wasilisho kuhusu
Maslahi ya Taifa kwa Watumishi wa Ofisi ya Rais, UTUMISHI Mtumba, Jijini
Dodoma.
Ameongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora ni muhimu kwa ustawi wa Taifa la Tanzania kwa kuwa
inasimamia rasilimaliwatu, hivyo, Watumishi wake wanatakiwa kufanya uamuzi
wakati wote kwa kuzingatia uadilifu, falisafa ya nchi, uwezo wa nchi kiuchumi,
rasilimali zilizopo na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Amewasisitiza pia Watumishi kupendekeza jambo la
maendeleo kwa kuzingatia miongozo na kufuata ngazi za madaraka, uzalendo na hatimaye
viongozi waweze kufanya uamuzi kwa kwa kuzingatia ilani ya chama husika na Maslahi
mpana ya taifa.
“Ni fahari kubwa kuitumikia nchi yako kwa umahiri na uwezo
mkubwa na epuka kuwa na kinyongo unapotekeleza majukumu ya Kitaifa kwa kuwa maslahi
ya taifa yanaanzia kwa mtu binafsi” Dkt. Kanuwa.
Akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi
hao, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala Bw. Musa
Magufuli alimshukuru Dkt. Kanuwa kwa kutoa elimu hiyo kwa watumishi wake na ameahidi
kuchukua wasilisho hilo na kulisambaza kwa watumishi wote ili waendelee
kujifunza ingawa haitaondoa dhana ya kuita wawezeshaji kutoa elimu hiyo.
Mafunzo hayo ni mwendelezo wa utaratibu uliowekwa na
Ofisi hiyo wa kutoa uelewa kuhusu masuala mbalimbali katika Utumishi wa Umma
ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika
katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya
kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika
katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli (wa pili kutoka
kushoto) akizungumza jambo na muwasilisha mada Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Taaluma Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.
Salim Ahmed Salim, Dkt. Juma Kanuwa (wa kwanza kushoto) mafunzo ya kuwajengea
uwezo watumishi wa ofisi hiyo
yaliyofanyika katika Mji wa
Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Aliyekaa kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi.
Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Taaluma Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.
Salim Ahmed Salim, Dkt. Juma Kanuwa akifanya wasilisho kuhusu Maslahi ya
Taifa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi
wa
Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa
Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Taaluma Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.
Salim Ahmed Salim, Dkt. Juma Kanuwa (hayupo pichani) wakati akifanya wasilisho kuhusu Maslahi ya Taifa kwa watumishi hao walipokuwa kwenye mafunzo ya kuwajengea
uwezo katika masuala ya utendaji kazi.
Mtumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala
Bora, Bw. Deogratias Kawogo
(aliyesimama) akiwasilisha
hoja wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika utendaji kazi
yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya
kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika
katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment