Na. Veronica Mwafisi-Serengeti
Tarehe 03 Oktoba, 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka viongozi wa Mkoa wa Mara kutekeleza miradi ya maendeleo kwa usahihi ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kutumika kikamilifu na wananchi.
Akizindua mradi wa Zahanati ya
Getarungu uliofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani kupitia Shirika ya
Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) leo tarehe 3 Oktoba, 2024 wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na
kusikiliza changamoto za wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani
Mara, amesema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa zahanati hiyo na kutaka
halmashauri za mkoa huo kuiga utekelezaji wa namna hiyo.
“Nimefurahi
sana, kupitia ziara hii nzuri, kubwa nililojifunza ni utekelezaji wa miradi kwa
usahihi sana, tujifunze na sisi halmashauri kuangalia miradi inayotekelezwa kwa
usimamizi mzuri inavyokuwa na je sisi tunashindwa wapi? Mhe. Simbachawene
ameuliza
Amesema
mradi huo wa zahanani ya Getarungu umesimamiwa na Mkandarasi Maalum na umekuwa ni wa kuridhisha sana, lakini kwenye
halmashauri ambako Wakandarasi wanalipwa mishahara, miradi yao inakuwa sio ya
kuridhisha.
“Nimezindua
zahanati hii ya Getarungu kwa kujidai sana, ni nzuri inafurahisha, nawasisitiza
viongozi katika halmashauri kuiga mfano huu mzuri, tukiendelea kutosimamia kwa
usahihi tutachukuliana hatua.” Mhe. Simbachawene amesisitiza
Amesema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya jitihada za kukuza sekta ya utalii, kuongeza pato la taifa kupitia sekta ya utalii na kujenga mahusiano mazuri na wadau wa maendeleo na ndio sababu ya kupatikana kwa mradi huu wa zahanati 8 kwa mara moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ikiwemo hiyo aliyoizindua leo ya Getarungu.
Mhe.
Simbachawene ameendelea na ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika Mkoa wa Mara, ambapo
leo ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Butiama na kuzindua
miradi mbalimbali ikiwemo zahanati ya Getarungu, barabara ya kituo kipya cha
mabasi Koreri na Shule ya Msingi Chief
Manyori.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akizungumza na wananchi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Serengeti baada ya kuzindua Zahanati ya Getarungu iliyopo kata
ya Nyansurura wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na
kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi akitoa neno la shukrani
kwa Serikali kutokana na miradi ambayo imeitekeleza katika mkoa wake wakati wa
ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Mwonekano wa vitanda
vya wagonjwa vitakavyotumika katika Zahanati ya Getarungu iliyokaguliwa na kuzinduliwa
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
katika Zahanati
ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Baadhi
ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
(aliyesimama kushoto)
wakati akizungumza nao baada ya kukagua na kuzindua Zahanati ya Wilaya ya Serengeti
wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyevaa miwani) akisikiliza
changamoto ya kiutumishi kutoka kwa Mhe. Diwani Bw. Josephat Seronga (aliyevaa kofia)
wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akisisitiza jambo baada ya kukagua vitanda vya wagonjwa kwenye Zahanati
ya Getarungu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti wakati wa ziara yake ya
kikazi katika mkoa wa Mara iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Mwonekano wa nyuma wa Zahanati ya
Getarungu iliyopo katika Halmashauri
ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara ambayo imekaguliwa na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa ziara yake ya kikazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Bi. Kemirembe Lwota baada ya
kuwasili katika Wilaya hiyo kwa lengo la kukagua na kuzindua Zahanati ya
Getarungu iliyopo katika Halmashauri
hiyo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na wananchi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambayo aliikagua na
kuizindua wakati wa
ziara yake
ya kikazi mkoani Mara.
Mwonekano wa vyoo vya Zahanati ya Getarungu iliyopo katika
Halmashauri
ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara ambavyo vimekaguliwa na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
wakati wa ziara yake ya kikazi.
No comments:
Post a Comment