Thursday, October 3, 2024

MHE. SIMBACHAWENE AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA STENDI MPYA KORERI

 HABARI KATIKA PICHA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikata utepe na kuweka  jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya stendi mpya Koreri iliyopo Kijiji cha Matare-Mugumu wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Dkt. Amsabi Mrimi wakati akitoa shukrani kwa waziri huyo baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya stendi mpya Koreri iliyopo Kijiji cha Matare-Mugumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti. Wengine ni Viongozi wa Mkoa wa Mara na Wananchi wa Halmashauri hiyo.

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyenyoosha mkono) akitazama mchoro unaoonesha kabla na baada ya ujenzi wa barabara ya stendi mpya Koreri kabla ya Waziri huyo kuweka jiwe la msingi wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.


No comments:

Post a Comment