Na. Veronica Mwafisi-Rorya
Tarehe 02 Oktoba, 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amezindua Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri huku akiwasisitiza wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii kwa maendeleo yao ya baadae na taifa kwa ujumla.
Mhe. Simbachawene amesema hayo leo
tarehe 2 Oktoba, 2024 wakati wa ziara yake ya kikazi
ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za
wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara ikiwa ni siku yake
ya pili ya kukagua utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo katika mkoa huo.
Waziri
Simbachawene amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi mingi ikiwemo ya elimu hivyo ili
kuunga mkono jitihada za Rais, wanafunzi hao hawana budi kusoma kwa bidii.
“Shule
nzuri namna hii kujengwa kijijini ni maendeleo makubwa yaliyofanywa na Serikali
ya Awamu ya Sita, hivyo ni wajibu wenu ninyi wanafunzi kusoma kwa bidii kwa
maendeleo yenu na taifa kwa ujumla,’’Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Ujenzi
wa Shule ya Sekondari Ingri umeigharimu Serikali kiasi cha shilingi milioni 584
mpaka kukamilika kwake ambapo inajumuisha madarasa, maabara, chumba cha TEHAMA
na Maktaba.
Ujenzi
wa shule hiyo umewaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi hao na
kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule waliokuwa wakisoma awali.
Mhe.
Simbachawene amewasisitiza wanafunzi na watumishi wa shule hiyo kutunza majengo
na vifaa vyote vilivyomo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Simbachawene amezindua ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya utakaotumika kufanya shughuli mbalimbali kwa maendeleo ya Halmashauri hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri mara baada ya kuwasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya
kwa lengo la kuzindua shule hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani
Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipiga makofi mara
baada ya kuweka jiwe la msingi katika Ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya Rorya wakati wa ziara
ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga
kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara. Aliyevaa
kofia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Kanali Evance Mtambi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Wa pili kutoka kushoto) akisisitiza
jambo wakati akielekea kuweka jiwe la msingi katika Ukumbi wa Halmashauri ya
Wilaya Rorya alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Kanali Evance Mtambi na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Dkt. Khalfan
Haule.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri mara baada ya kuzindua
shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya wakati wa ziara yake
ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya
Rorya, Dkt. Khalfan Haule wakati akifafanua jambo kuhusu Shule ya Sekondari ya
Kutwa Ingri kabla ya Waziri huyo kuzindua Shule hiyo iliyopo Halmashauri ya
Wilaya ya Rorya.
Mwonekano wa ukumbi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya uliowekwa jiwe la msingi na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani
Mara.
Mwonekano
wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri iliyozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene
alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akivalishwa skafu na vijana wa Skauti
mara baada ya kuwasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kwa lengo la kukagua na kuzindua utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment