Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 10 Oktoba, 2024
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji ya
Rasilimaliwatu utaisaidia Serikali kufanya msawazo katika Utumishi wa Umma ili
kuwa na mtawanyo mzuri wa watumishi kwa lengo la kuboresha utendaji katika
utumishi wa umma.
Bw.
Mkomi ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha kujadili matokeo ya tathmini ya mahitaji ya
rasilimaliwatu katika utumishi wa umma kwa Wakurugenzi
wa Idara za Utawala na Usimamizi
wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara zote, wataalamu wanaosimamia uandaaji na ujazaji wa
mahitaji ya watumishi kutoka wizara zote pamoja na Wakurugenzi na wataalamu
kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI.
Bw.
Mkomi amesema kila Mkurugenzi
anafahamu umuhimu wa mahitaji ya rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma na kuwasihi wafanye tathmini ya kutosha.
“Ukisema
una watumishi wachache, tutakuuliza unahitaji watumishi wangapi? kwani
unatakiwa uwe umefanya tathmini ya kutosha kwasababu inawezekana kumhitaji
kwako mtumishi au kutokumhitaji kunatokana na matakwa yako na si mfumo
unaokufahamisha kuwa mtumishi huyu ni wa ziada.” Bw.
Mkomi amesema.
Bw. Mkomi amesema msawazo katika utumishi wa umma unahitajika
kufanywa katika maeneo mawili ikiwemo mjini ili kutokuwa na watumishi wa ziada
ambao hawana majukumu ya kutosha katika maeneo yao ya kazi lakini pia msawazo
huo utasaidia kuunganisha familia.
Bw. Mkomi ameongeza kuwa, msawazo hautaweza kufanyika
bila kuwa na taarifa halisi ya mahitaji na idadi ya watumishi waliopo katika
maeneo husika hivyo, ni vizuri washiriki wakaangalia namna ya kufanya kwani
inatakiwa kujua watumishi wangapi wanahitajika wapi, wakafanye nini na baada ya
kujua hayo itapatikana nafasi nzuri ya kuboresha.
“Niwatake mshiriki kikamilifu kwa
kuipokea taarifa hiyo, kuichambua na kutoa mapendekezo
yatakayosaidia kuboresha Mfumo huo
utakaowezesha kuwa na mtawanyo
mzuri wa watumishi katika Taasisi za Umma.” Bw. Mkomi amesisitiza.
Akitoa
neno la utangulizi, Mkurugenzi wa Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda
ameelezea lengo la kikao kazi hicho kuwa ni kujadili matokeo ya tathmini ya Rasilimaliwatu katika
Taasisi za Umma ili kupata maoni toka kwa wadau hao na kuboresha mfumo huo katika
Utumishi wa Umma kwa masilahi mapana ya taifa.
Kikao
kazi hicho kilichoanza leo kinafanyika kwa muda wa siku mbili ambapo mada mbalimbali
zitawasilishwa ikiwemo Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma, matokeo ya Wizara na vigezo kwa upande
wa Wizara na Makundi ya Taasisi.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akifungua
kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi
wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo
ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.
Sehemu ya Wakurugenzi
wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka
serikalini wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo
pichani) wakati akifungua kikao kazi kilicholenga
kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda akitoa
neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma
Mkomi (hayupo pichani) kufungua kikao kazi cha Wakurugenzi
wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka
serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kulia) akiwa katika kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kabla ya
kufungua kikao hicho kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo. Kulia
kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya
Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco
Kipanda
Baadhi
ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakati
akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini
kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi
wa Umma jijini Dodoma leo.
Baadhi ya Maafisa kutoka
Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakati akifungua
kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na
Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya
Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala
na Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Felista Shuli akijibu moja ya
hoja iliyowasilishwa wakati wa kikao kazi cha
Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi
kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki
wa kikao kazi cha Wakurugenzi
wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka
serikalini mara baada ya kufungua kikao hicho kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini
ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya
Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda.
Sehemu ya washiriki
wa kikao kazi cha kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo
pichani) wakati akifungua kikao kazi hicho kilichofanyika
jijini
Dodoma leo.
Afisa Tawala Mwandamizi, Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Waziri
Mkumbo akiwasilisha mada kwa Wakurugenzi wa Idara za
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kuhusu Matokeo ya
Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakati wa kikao
kazi cha kujadili matokeo ya tathmini hiyo kilichofanyika jijini
Dodoma leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Kilimo, Bw. Philbert Lutale akichangia
mada wakati wa kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili
Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini
Dodoma leo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Fedha, ambaye ni
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Idara ya Rasilimaliwatu wa Wizara
zote, Bw. Lusius Mwenda (kulia) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha Wakurugenzi
hao na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini
ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini
Dodoma leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya
Uendelezaji wa Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda.
No comments:
Post a Comment