NA. LUSUNGU HELELA-DODOMA
SERIKALI imeonya ukiukwaji wa maadili kwa watumishi wa umma ikiwemo mmomonyoko wa maadili ikiwemo viashiria vya mapenzi ya jinsia moja na mavazi yasiyofaa kwa watumishi wa umma jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya serikali.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 17,2024 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma.
Bw.Daudi amesema kuwa Ofisi imeanza kupokea tuhuma na malalamiko kuhusu kuwepo kwa viashiria vya mmomonyoko wa Maadili kinyume na mila na desturi za nchi yetu vinavyohusu vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa baadhi ya watumishi wa umma.
Amesema kuwa, vitendo hivyo ni miongoni mwa
vitendo vya kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi lakini pia ni vitendo vya
kinyume na maadili kwa mujibu wa miongozo ya utumishi wa umma.
“Hivyo, tumieni kikao kazi hiki, kujadili na kubadilishana uzoefu ili kuja na mapendekezo ya namna sahihi ya kudhibiti vitendo hivi na namna sahihi ya kushughulikia masuala haya yatakapojitokeza katika maeneo yenu ya kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohusishwa navyo ili kuepuka kuchafua taswira ya utumishi wa umma kwa ujumla,”amesema Bw.Daudi
Aidha ameziomba taasisi za Dini nchini kusimamia maadili na kuonya na kukemea vitendo hivyo vya ndoa ya jinsia moja katika jamii ya kitanzania mana wao wana nguvu na Sauti kubwa ya kusikika zaidi.
“Hivi sasa zipo nchi zimeacha kuzaliana kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo vya mapenzi ya jinsia moja,,Tanzania hatutaki kufika huko ndio mana tunakemea,”amesema
Kuhusu mavazi yasiofaa ameelekeza watumie waraka namba 6 wa utumishi wa umma unaozungumzia mavazi kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaochafua taswira ya serikali kwa kuvaa hovyo ndani na nje ya utumishi.
Amesema kuwa zipo taasisi ambazo viongozi wake wameanza kulegalega kwa kutochukua hatua na kuacha watumishi wakivaa mavazi kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.
“Nawaagiza kutumia waraka namba sita
nasisitiza kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaovaa mavazi yasiyofaa na
kuweka mkazo katika hilo , msisite kuchukua hatua mana yanachafua taswira nzima
ya utumishi wa umma,”amesema
Amesema Ofisi imekuwa ikipokea mrejesho kutoka kwa wananchi tunaowahudumia, kuhusu hali isiyoridhisha ya mavazi kwa watumishi wetu wa umma.
Kwa msingi huo, tumieni kikao hiki kupitia Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 6 wa mwaka 2020 kuhusu Mavazi kwa Watumishi wa Umma, ili kujengeana uwelewa wa pamoja kupitia uzoefu mtakaobadilishana baina yenu kuhusu utekelezaji wa Waraka huo kwa watumishi waliopo kwenye maeneo yenu,.
“Na muweze kuchukua hatua ipasavyo kwa wanaokiuka Waraka husika ikizingatiwa kuwa, mwonekano wa watumishi wa umma wanapotoa huduma unabeba taswira ya taasisi, utumishi wa umma na Serikali kwa ujumla;,”amesema
Aidha amewataka Watumishi wa umma wa kada za afya na ardhi kuachana na vitendo vilivyo kinyume na maadilii ya taaluma zao ikiwemo rushwa na kuwajibu vibaya wananchi wakati wa utoaji wa huduma.
Amesema kuwa kumekuwepo na taarifa za malalamiko mengi
kutoka vyanzo mbalimbali, yatokanayo na vitendo vya ukikuwaji wa maadili ya
utendaji na maadili ya kitaaluma katika utumishi wa umma.
“Malalamiko hayo yamekuwa yakiwahusisha baadhi ya
watumishi wetu wa umma kutoka kada mbalimbali wakiwepo Wauguzi,
Madaktari, Waalimu, Maafisa Utumishi, Maafisa Ardhi, Wahasibu katika
Halmashauri, Wataalam waliopo Sekta ya Ugavi wa Umeme, na Maji, pamoja na
Wahandisi wanaosimamia miradi ya maendeleo. “amesema
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Maadili,Bw.Ally Abdul Ngowo,amesema wanatarajia kupokea taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha Septemba 2023 hadi Septemba 2024 katika maeneo yao kuhusu suala la maadili.
“Kwa hiyo Kila Taasisi au Kila mshiriki atapata nafasi kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wake na amefanya nini katika eneo lake kuhusu suala la maadili katika kipindi hicho.”amesema
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.Xavier Daudi akizungumza wakati akifungua Kikao kazi cha kubadilisha uzoefu wa masuala ya Maadili na Utawala Bora baina ya Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Maamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma kilichofanyika leo Jijini Dodoma
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Maadili,Bw.Ally Ngowo,akizungumza wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 17 had 18,2024 jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli (kulia) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi, wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika leo jijini Dodoma
Sehemu ya Washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi, wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika leo jijini Dodoma
NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 17 had 18,2024 jijini Dodoma
NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akizungumza na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli akiwa ameambatana na baadhi ya Wakurugenzi mara baada ya kufungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 17 had 18,2024 jijini Dodoma
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Maadili,Bw.Ally Ngowo,akizungumza na vyombo vya habari mara baad ya kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 17 had 18,2024 jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment