Thursday, October 3, 2024

WAZIRI SIMBACHAWENE: SERIKALI INAYOONGOZWA NA RAIS. DKT SAMIA SULUHU HASSAN IPO MAKINI KUHAKIKISHA MAENDELEO YANAMGUSA KILA MWANANCHI KUPITIA MIRADI

 HABARI KATIKA PICHA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama baada ya kukagua na kuzindua Shule ya Msingi Chief Manyori iliyopo katika Kijiji cha Nyamisisye wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Mara.


Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene baada ya Waziri huyo kukagua na kuzindua Shule ya Msingi Chief Manyori iliyopo katika Kijiji cha Nyamisisye wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Mara.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi baada ya kuwasili katika Shule ya Msingi Chief Manyori wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.


Mwonekano wa moja ya majengo ya shule ya Chief Manyori iliyokaguliwa na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.


Baadhi ya Wanafunzi wanaosoma katika shule za Halmashauri ya Wilaya ya Butiama wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza kwenye ziara yake ya kikazi liyolenga kukagua na kuzindua shule ya Msingi Chief Manyori iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiteta jambo na Mbunge wa Butiama, ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Jumanne Sagini wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara.


Mwonekano wa jengo la utawala lililopo katika Shule ya Msingi Chief Manyori katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara ambalo limekaguliwa na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Butiama mkoani Mara. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi. 


No comments:

Post a Comment