Na. Lusungu Helela - Dodoma
Serikali imesema itaendelea kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa umma wanaothibitika kukiuka maadili ya utumishi wa umma huku ikiahidi kuwekeza zaidi katika matumizi ya TEHAMA ili kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Maadili
Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw.Juma Mkomi ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akifunga Kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Maadili na Utawala Bora baina ya Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma.
Amesema watumishi wala rushwa na walevi na wenye tabia na mienendo isiyofaa kwenye jamii haitawafumbia macho
‘’Hivi karibuni nimewahamisha watumishi wanne kutoka wizara fulani wanaotuhumiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
‘’ Kuna baadhi ya watumishi wanalala baa na asubuhi wanakwenda kazini wakiwa wachovu na hawajapiga mswaki na hivyo kuwapa shida wananchi wanapowahudumia’’ ameng’aka Katibu Mkuu Mkomi
Amesema dhana ya utumishi wa umma ni maadili na bila maadili hakuna utumishi wa umma hivyo Serikali itaendelea kufanya tahtmini kwa kina kuhusu tabia na mienendo ya watumishi wa umma wakati wote.
Kufuatia hatua hiyo Mkomi amesema watumishi wapya watakaokuwa wakiajiriwa wataanza kufanyiwa upekuzi wa kutosha kuhusu tabia na mienendo yao kulingana na majukumu na miiko ya taaluma zao ili kuwa na utumishi wenye taswira nzuri
Katika hatua nyingine Mkomi amewataka Waajiri kuimarisha mifumo madhubuti na taratibu za kuwalinda watoa taarifa juu ya vitendo vya ukiukwaji wa maadili na rushwa mahali pa kazi
Amesema kumeibuka tabia za baadhi ya waajiri kushindwa kuwalinda watoa taarifa pindi mnapoletewa taarifa ya vitendo vya ukiukwaji maadili, hii sio sawa walindeni hao ni watu muhimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi akizungumza wakati akifunga Kikao kazi
cha kubadilisha uzoefu wa masuala ya Maadili na Utawala Bora baina
ya Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za
Maadili ya Kitaaluma kilichofanyika kwa
muda wa siku mbili jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi akiwa katika picha ya pamoja na
Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
mara baada ya kufunga kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili
na utawala bora baina ya Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Mamlaka
Simamizi za Maadili ya Kitaluma, kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.Juma Mkomi ,
wakati akifunga kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili
na utawala bora baina ya Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi
za Maadili ya Kitaluma, kinachofanyika kwa muda wasiku mbili jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment