Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam
Tarehe 18 Oktoba, 2024
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameipongeza kwaya ya Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania (TPSC) kwa kuimba nyimbo zinazobeba uzalendo wa taifa la
Tanzania.
Mhe. Sangu ameyasema hayo leo katika Ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuizindua
rasmi kwaya hiyo na kuongoza harambee ili iweze kujiimarisha.
Mhe. Sangu amesema amekuwa asikiliza mara kwa mara
nyimbo za kwaya hiyo kwasababu zimekuwa zikielimisha masuala mbalimbali yaliyofanyika
katika nchi hii ikiwemo suala ya uzalendo.
“Mimi ni shabiki mkubwa wa kwaya hii kabla hata ya
kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwani
licha ya kuburudisha imekuwa ikiimba nyimbo za uzalendo, maadili, historia ya
nchi yetu na ikielezea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
iliyofanywa na viongozi wa nchi yetu toka awamu ya kwanza mpaka sasa.” Mhe.
Sangu.
Mhe. Sangu ameongeza kuwa, pamoja na changamoto
mbalimbali zinazoikabili kwaya hiyo ikiwemo ukosefu wa studio ya kurekodi na chombo
cha usafiri lakini wamekuwa wakishiriki katika matukio mbalimbali na kuweza
kutekeleza majukumu yao ya kuburudisha, kuelimisha, kufundisha na kuonya.
Ameupongeza uongozi wa TPSC kwa kuongoza na kuisimiamia
vizuri kwaya hiyo ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika matukio mbalimbali
yakiwemo ya Serikali.
Katika hatua nyingine Mhe. Sangu amewahimiza wanakwaya
na washiriki wengine katika hafla hiyo kujiandikisha katika daftari la wapiga kura
ili washiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndio kipaumbele cha
taifa kwa sasa, Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha mfano na
kujiandikisha, hivyo nawasihi wote wenye sifa tujiandikishe ili tuchague
viongozi wanaofaa kwa muskabali wa taifa letu. Mhe. Sangu amesisitiza.
Awali kabla ya kumkaribisha Naibu waziri Sangu
kuzindua kwaya hiyo na kuongoza harambee, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa
TPSC, Dkt. Ernest Mabonesho alisema vijana wa kwaya hiyo wamekuwa wazalendo na
waadilifu sana katika kulitumikia taifa licha ya changamoto walizo nazo katika
uendeshaji wa kwaya hiyo.
Dkt. Mabonesho ametoa shukrani kwa Viongozi wa Ofisi
ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa miongozo na maelekezo mbalimbali ambayo
wamekuwa wakiyatoa katika kuiimarisha kwaya hiyo na kuomba kuendelea kuisadia.
Albam yenye jumla ya nyimbo 25 imezinduliwa na kiasi
cha shilingi milioni 123 kimechangwa katika hafla hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na waalikwa mbalimbali na wanafunzi wa Chuo cha Utumishi
wa Umma Tanzania walioshiriki kwenye uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya chuo hicho iliyofanyika
katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wanafunzi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Deus Sangu wakati wa uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya chuo hicho iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa TPSC, Dkt. Ernest Mabonesho
akitoa neno la
utangulizi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) kabla ya kumkaribisha kuzungumza na
waalikwa mbalimbali na wanafunzi wa chuo cha TPSC wakati wa uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya chuo hicho iliyofanyika katika
Ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu wakati wa uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya chuo hicho iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Deus Sangu akiwa ameshika mfano wa hundi
ya fedha iliyochangiwa na ofisi hiyo wakati wa uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania iliyofanyika
katika Ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam. Wengine ni Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala
Bora.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (wa pili kushoto) akipokelewa
na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda (wa kwanza
kulia) mara baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili Ukumbi
wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzindua harambee ya
Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania. Katikati ni Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho.
Wanakwaya wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
wakiimba wakati wa uzinduzi wa harambee ya kwaya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akipokea zawadi ya
flashi za baadhi ya Viongozi wa Nchi zenye nyimbo 25 za Kwaya ya Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania wakati wa uzinduzi wa harambee ya kwaya hiyo
iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Deus Sangu akiwashukuru wanakwaya wa Manispaa ya Ubungo mara baada ya
kuchangia fedha wakati wa uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment