Na. Veronica Mwafisi-Moshi
Tarehe 26 Oktoba, 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesisitiza watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) kutumia kikamilifu vitendea kazi ambavyo serikali imekuwa ikiwapatia ili kuhakikisha kazi ya kupambana na rushwa inatekelezwa kwa ufasaha.
Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo
leo tarehe 26 Oktoba, 2024 katika Shule ya Polisi-Moshi alipokuwa akitoa maelezo ya awali
kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa kufunga mafunzo ya awali kwa watumishi wapya 436
wa TAKUKURU.
Mhe.
Simbachawene amesema katika kuhakikisha rushwa inatokomezwa nchini, Serikali
imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kujenga Ofisi za TAKUKURU mikoani
na wilayani, kuajiri watumishi na kutoa vitendea kazi, hivyo hakuna kisingizio tena kwa watumishi hao
kutofanya kazi kwa ufasaha.
“Hakuna kisingizio tena, ninyi
leo mmekuwa mashahidi na kuona Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa alivyokuwa
akikabidhi magari kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yenu ya kupambana na
rushwa, hivyo mkavitendee haki vitendea kazi hivyo kwa kufanya kazi kwa bidii
na uadilifu” Mhe. Simbachawene.
Waziri
Simbachawene amemuahidi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuwa yeye pamoja na
watendaji wa Ofisi yake wataendelea kuisimamia kikamilifu taasisi hiyo na
kuvitumia vizuri vitendea kazi wanavyopatiwa katika jukumu la kuzuia na
kupambana na rushwa.
Waziri
Simbachawene amemshukuru Waziri Mkuu kwa kufunga mafunzo hayo na kuwapongeza
wahitimu pamoja na wote walioshiriki katika kufanikisha mafunzo hayo ya Maafisa
Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi.
Mafunzo
hayo yaliyolenga kuwaandaa watumishi wa TAKUKURU kutekeleza majukumu yao kwa uzalendo,
uadilifu, weledi, uwajibikaji na ushirikiano yamefanyika kwa muda wa miezi
mitano (5) na yamefungwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila (kulia) funguo ya gari ishara ya kukabidhi magari 88 kwa TAKUKURU akimwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuboresha utendaji kazi. Wa kwanza kushoto anayeshuhudia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa akizungumza na wahitimu Maafisa Uchunguzi na
Wachunguzi Wasaidizi wa TAKUKURU (hawapo pichani) wakati akifunga mafunzo
ya awali ya uchunguzi kwa maafisa hao katika hafla iliyofanyika Chuo cha Polisi Tanzania, mjini Moshi.
Sehemu ya wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi
na Wachunguzi
Wasaidizi wa TAKUKURU wakimsikiliza Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo ya awali ya uchunguzi
kwa maafisa hao katika hafla iliyofanyika Chuo cha Polisi Tanzania, mjini Moshi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa (hayupo pichani) kuzungumza na
kufunga mafunzo kwa wahitimu Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi
Wasaidizi wa TAKUKURU wakati wa hafla
iliyofanyika Chuo cha Polisi Tanzania, mjini Moshi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila (kushoto) wakati wa kufunga
mafunzo ya wahitimu Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wa TAKUKURU yaliyofanyika katika Chuo cha Polisi Tanzania mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (katikati) akikata utepe ishara ya kukabidhi magari 88 kwa TAKUKURU akimwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuboresha
utendaji kazi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua grawide la wahitimu Maafisa Uchunguzi
na Wachunguzi Wasaidizi wa TAKUKURU mara baada ya kuwasili Chuo cha Polisi Tanzania mjini Moshi kwa ajili ya kufunga mafunzo hayo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama
(katikati) akifuatilia jambo wakati wa kufunga mafunzo ya wahitimu Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wa TAKUKURU yaliyofanyika katika Chuo cha Polisi Tanzania mjini
Moshi.
Sehemu ya wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wa TAKUKURU wakila kiapo mara
baada ya kuhitimu mafunzo ya awali ya uchunguzi kwa maafisa hao katika hafla iliyofanyika Chuo cha
Polisi Tanzania, mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa (kulia) akimkabidhi
cheti mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri wakati wa
mafunzo ya awali ya uchunguzi kwa maafisa hao katika Chuo cha Polisi Tanzania, mjini Moshi.
Sehemu ya wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wa TAKUKURU wakipita kwa gwaride mwendo wa pole mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa kufunga
mafunzo ya awali ya uchunguzi kwa maafisa hao katika Chuo cha Polisi Tanzania, mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa (Wa pili kutoka kushoto) akipokea vitendea kazi vya TAKUKURU kutoka
kwa Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila (Wa kwanza kulia).
No comments:
Post a Comment