Na. Mwandishi Wetu.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora SACP. Ibrahim Mahumi amesema matokeo ya jumla ya Zoezi la Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kupitia Mfumo wa Human Resources Assessment System (HRA) yanaonesha kuwa kuna upungufu wa Watumishi katika Utumishi wa Umma, ingawa katika upungufu huo bado kuna Idara na Vitengo ndani ya baadhi ya Taasisi za Umma zina ziada ya Watumishi.
SACP. Mahumi amesema hayo Oktoba 17, 2024 wakati akifungua Kikao Kazi cha Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali kinachojadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
Amesema kuwa, Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ilifanya zoezi la kuthmini ya mahitaji ya rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kupitia Mfumo wa Human Resources Assessment System (HRA) kwa lengo la kubaini Watumishi waliopo na wanaohitajika katika Utumishi wa Umma ambapo jumla ya Taasisi 534 kati ya 571 zilizopo katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara iilifikiwa.
Aidha, amefafanua kuwa taarifa hiyo inaonesha jitihada kubwa ambazo zimefanywa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwenye usimamizi wa rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kwa kuwa Serikali imekuwa na uwezo wa kubaini idadi ya Watumishi waliopo na wanaohitajika katika Utumishi wa Umma kwa miaka mitano ijayo.
“Ni imani yangu kuwa mtashiriki katika kujadili, kutoa maoni na ushauri ili kuweza kuboresha Taarifa ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kwa maslahi mapana ya usimamizi na ukuaji wa Utumishi wa Umma” amesema SACP. Mahumi.
Awali,
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Bi. Veila Shoo amesema kuwa, Taarifa itakayowasilishwa kwa washiriki
katika kikao kazi hicho ni matunda ya kazi ya washiriki iliyofanyika kwenye
Taasisi wanazotoka.
Pia,
alitumia fursa ya kikao kazi hicho kuwashukuru Wakuu wa Taasisi wote waliotoa
ushirikiano stahiki wakati zoezi ambapo matokeo yake yameonekana na Serikali
inayafanyia kazi.
Kikao
kazi cha kujadili matokeo ya zoezi la tathmini ya mahitaji ya rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma kinafanyika kwa siku mbili tarehe 17 na 18 Oktoba, 2024
katika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment