Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 23 Machi, 2022
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama
amekagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za kudumu za Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora unaoendelea katika Mji wa Serikali-Mtumba
na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa.
Mhe. Jenista ameridhishwa
na maendeleo ya ujenzi wa ofisi hiyo mara baada ya kufanya ukaguzi na kuielekeza
Menejimenti ya ofisi yake kuhakikisha inasimamia kikamilifu ili ofisi yake iwe
ya kwanza kukamilisha ujenzi na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mhe. Jenista amesema,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ilipata bahati
ya kuwekwa kwa jiwe la uzinduzi wa ujenzi wa ofisi za wizara zote katika Mji wa
Serikali, hivyo ni vema kuilinda heshima hiyo kwa kuwa wa kwanza kukamilisha
ujenzi wa ofisi hizo.
“Nimeridhishwa na
maendeleo ya ujenzi kwani kazi inaonekana kuwa ni bora na hata taarifa ya
Mshauri Elekezi inaeleza kuwa viwango vya ujenzi vina ubora unaokubalika na
unaoendana na thamani ya fedha inayotolewa na Serikali.” Mhe. Jenista ameongeza.
Mhe. Jenista
amempongeza Mkandarasi, Mshauri Elekezi na Menejimenti ya ofisi yake kwa kuendelea
kusimamia vizuri ujenzi wa ofisi hizo.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro
ameungana na Mhe. Jenista Mhagama kumpongeza Mkandarasi ambaye ni Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) na Mshauri Elekezi Watumishi Housing kwa kazi nzuri
waliyoifanya ambayo imefikia hatua inayoridhisha.
Dkt. Ndumbaro amewataka
TBA na Watumishi Housing kuendelea na kasi hiyo ya ujenzi ili kutekeleza
maelekezo ya Mhe. Waziri ya kutaka ofisi yake kuwa ya kwanza kukamilisha ujenzi
pamoja na azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kutaka wizara zote kukamilisha
ujenzi wa ofisi zake katika Mji wa Serikali Mtumba.
Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa aliweka jiwe la uzinduzi wa
ujenzi wa ofisi za wizara zote awamu ya pili katika Mji wa Serikali Mtumba
jijini Dodoma tarehe 2 Desemba, 2021 kwenye eneo linalojengwa Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza na Mkandarasi ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA) na Mshauri Elekezi Watumishi Housing (WHC) wanaojenga jengo
la ofisi za kudumu za Ofisi ya Rais - UTUMISHI alipoenda kukagua maendeleo ya
ujenzi wa jengo hilo kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Wa kwanza
kulia ni Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa pongezi na kuwasisitiza Mkandarasi ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Mshauri Elekezi Watumishi Housing (WHC) wanaojenga jengo la ofisi za kudumu za Ofisi ya Rais - UTUMISHI na kufikia hatua kubwa wakati Waziri wa Ofisi yake Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Mshauri
Elekezi wa mradi (WHC), Mhandisi Lwitiko Mwandobo akitoa taarifa ya maendeleo
ya mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi za kudumu za Ofisi ya Rais - UTUMISHI wakati
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo kwenye Mji wa
Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akielekea kukagua jengo la ofisi za kudumu za Ofisi ya Rais -
UTUMISHI linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Mtumba wakati Waziri
huyo alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo jijini Dodoma. Wapili kutoka
kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akikagua miundombinu ya jengo la ofisi za kudumu za Ofisi ya Rais
- UTUMISHI linaloendelea kujengwa na Mkandarasi ambaye ni
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Mshauri Elekezi Watumishi Housing
katika Mji wa Serikali Mtumba wakati Waziri huyo alipotembelea kuona maendeleo
ya ujenzi huo jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akishuka katika jengo la ofisi za kudumu za Ofisi ya Rais –
UTUMISHI linaloendelea kujengwa na Mkandarasi ambaye ni
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Mshauri Elekezi Watumishi Housing
(WHC) katika Mji wa Serikali Mtumba wakati Waziri huyo alipotembelea kuona
maendeleo ya ujenzi huo jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza na Katibu Mkuu wa ofisi yake wakati Waziri huyo
alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi za kudumu za Ofisi ya
Rais – UTUMISHI katika Mji wa Serikali Mtumba. Wengine ni baadhi ya Watendaji
wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Mkandarasi ambaye ni Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) na Mshauri Elekezi Watumishi Housing (WHC)
wanaojenga jengo hilo.
Muonekano
wa Jengo kubwa la kudumu la Ofisi ya Rais - UTUMISHI linaloendelea kujengwa na Mkandarasi
ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Mshauri Elekezi Watumishi Housing
(WHC) wanaojenga Jengo hilo wakati Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo kwenye Mji wa Serikali
Mtumba jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment