Tuesday, March 22, 2022

OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA YAWASILISHA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA BAJETI WA MWAKA 2022/2023 KWA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akizungumza wakati wa Kikao cha kuwasilisha Mpango wa Utekelezaji wa Bajeti wa mwaka 2022/2023 wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Taasisi zake leo jijini Dodoma.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati akiwasilisha Mpango wa Utekelezaji wa Bajeti wa mwaka 2022/2023 wa Ofisi yake Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha Mpango wa Utekelezaji wa Bajeti 2022/2023 wa Ofisi yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika Kikao kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwantumu Zodo akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Jenista Mhagama wakati akiwasilisha Mpango wa Utekelezaji wa Bajeti wa mwaka 2022/2023 wa Ofisi yake kwa Kamati hiyo Jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Prof. Palamagamba Kabudi akiwasilisha hoja mara baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuwasilisha Mpango wa Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi yake wa mwaka 2022/2023 jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Jenista Mhagama akijibu hoja iliyowasilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa Kikao cha kuwasilisha Mpango wa Utekelezaji wa Bajeti wa mwaka 2022/2023 wa Ofisi yake kilichofanyika Jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa Kikao cha kuwasilisha Mpango wa Utekelezaji wa Bajeti wa mwaka 2022/2023.

Baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa Kikao cha kuwasilisha Mpango wa Utekeleza wa Bajeti kwa mwaka 2022/2023. 



 


 



 











No comments:

Post a Comment