Na. Veronica
Mwafisi-Dodoma
Tarehe 28 Machi, 2022
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama ameielekeza Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) kuhakikisha wanayaishi maono ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya
kuhakikisha mipango na huduma za maendeleo zinawafikia wananchi kwa ukamilifu.
Mhe. Jenista
amesema hayo leo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti ya
TAKUKURU alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi wa taasisi hiyo.
Mhe. Jenista
amesema, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali anayoiongoza ya Awamu
ya Sita imejipanga kikamilifu kuleta mageuzi makubwa kwenye taifa katika sekta
zote ili wananchi wapate huduma bora na kwa wakati, hivyo, TAKUKURU wanao
wajibu wa kuhakikisha maono ya Mhe. Rais pamoja na Serikali ya Awamu ya Sita yanafikiwa
kwa ukamilifu.
“TAKUKURU
tuna deni kubwa sana kwa Watanzania katika kuhakikisha mipango na huduma
zinazotakiwa kuwafikia Watanzania zinawafikia kwa ukamilifu,” Mhe. Jenista
amesisitiza.
Ameongeza
kuwa, yale ambayo Watanzania wanafikiria Serikali yao iwafanyie, hayawezi
kufanikiwa kwa ufasaha kama miongoni kwa taasisi wezeshi ikiwemo TAKUKURU
isipofanya kazi yake sawasawa.
“Ili
taifa liweze kupiga hatua kimaendeleo, basi TAKUKURU katika kutekeleza majukumu
yetu ni lazima tuzingatie Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo
uliopo, maono ya Mhe. Rais aliyepo madarakani pamoja juhudi za Serikali ya
Awamu ya Sita katika kufanya mabadiliko makubwa ya mwenendo mzima wa uchumi,
upelekaji wa huduma kwa wananchi, nidhamu, maadili ya taifa hili,” Mhe. Jenista
amefafanua.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP.
Salum Hamduni amemshukuru Mhe. Waziri kwa kufanya nao kikao kazi na kuahidi
yeye pamoja na watendaji wengine kuyafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa ili
kuendana na matarajio ya Serikali ya kufikisha huduma bora kwa umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti hiyo
leo jijini Dodoma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye kikao na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti hiyo
kilichofanyika leo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi Salum Hamduni akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama kuzungumza na Menejimenti
ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa kikao kazi
chake na Menejimenti hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasili Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) leo wakati wa wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji
kwa watumishi wa taasisi hiyo. Aliombatana nao ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,
Kamishna wa Polisi Salum Hamduni na Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bi. Neema
Mwakalyelye.
Mkurugenzi wa Intelijensia –TAKUKURU, Bw. Malimi Mifuko akiwasilisha hoja
kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye kikao kazi chake na Menejimenti
hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) baada ya kumaliza kikao kazi chake na Menejimenti hiyo leo
jijini Dodoma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi za Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) makao makuu jijini Dodoma mara
baada ya kikao kazi chake na Menejimenti ya TAKUKURU.
No comments:
Post a Comment