Na. Veronica
Mwafisi-Njombe
Tarehe 19 Machi, 2022
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI), Mhe. Abdallah Chaurembo amempongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada
zake za kutafuta fedha kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Mhe. Chaurembo amesema hayo alipokuwa
katika ziara ya kikazi ya kamati yake
iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji
Njombe.
Mhe. Chaurembo amesema, Kamati yake
inamshukuru Mhe. Rais kwa kutoa fedha ambazo zimetekeleza Mradi wa ujenzi wa Zahanati
ya Mtaa wa Wikichi ambao umesogeza karibu huduma za afya kwa wananchi wa eneo
hilo.
Mhe. Chaurembo ameongeza kuwa, Kamati
yake imepokea taarifa kutoka kwa Mratibu wa TASAF wa eneo hilo pamoja na
kukagua zahanati hiyo iliyojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 89
iliyojumuisha na vifaa tiba, hivyo imeridhika kutokana na kazi nzuri
iliyofanyika.
Vilevile, Mhe. Chaurembo amempongeza
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. Ladislaus
Mwamanga kwa kupeleka wataalam ambao wamesimia vizuri ujenzi wa zahanati hiyo.
Mhe. Chaurembo amempongeza pia mratibu
wa TASAF kwa kusimamia vema fedha zilizotolewa na Mhe Rais kujenga Zahanati
hiyo ambayo imekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo na maeneo
jirani.
Sanjari na hilo, Mhe. Chaurembo
amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Wikichi kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika
kuhakikisha ujenzi wa Zahanati hiyo unakamilika kwa wakati.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na
Serikali za Mitaa (USEMI) inaendelea na ziara yake ya kikazi kukagua utekelezaji
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika Halmshauri ya Wilaya Mji
Njombe.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah
Chaurembo akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Wikichi wakati wa ziara ya
kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika
Halmashauri ya Mji Njombe.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha
Wikichi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na
Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Njombe.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) wakiongozana na Wananchi wa
Kijiji cha Wikichi kutazama Mradi wa ujenzi wa zahanati ya Wikichi wakati wa
ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF katika Halmashauri ya Mji Njombe.
Sehemu ya mwonekano wa jengo la Zahanati ya Wikichi iliyofadhiliwa na TASAF
pamoja na Michango ya Jamii. Zahanati hiyo imetembelewa na Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) wakati wa ziara ya kikazi ya
kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika
Halmashauri ya Mji Njombe.
No comments:
Post a Comment