Saturday, July 11, 2026

MHE. RIDHIWANI AWAASA WANAFUNZI “TABORA BOYS” KULINDA JINA ZURI LA SHULE YAO KWA KUJIEPUSHA NA TABIA ZISIZOFAA

Na. Veronica Mwafisi-Tabora

Tarehe 11 Julai, 2026

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewaambia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora kuishi katika maadili wawapo shuleni na hata baada ya kumaliza shule ili wajiepusha na tabia ambazo zitawafanya wajiingize katika makundi yasiyofaa ya uvunjivu wa amani.

 

Mhe. Ridhiwani amesema hayo leo tarehe 11 Julai, 2026 alipotembelea shule hiyo kabla ya kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Ualimu mkoani humo.

 

Amesema kuna maisha baada ya kumaliza shule, hivyo wanafunzi hao wanatakiwa wakawe mfano mzuri katika maadili na uzalendo kwa wengine huko wanakoenda kutokana na sifa za shule hiyo.

 

“Shule hii imetoa viongozi wengi sana, waadilifu na wazalendo, hivyo mtunze heshima yake, mkajitofautishe na wengine, msiige tabia ambazo sio nzuri,” amesisitiza.

 

Amepongeza uongozi wa shule hiyo kwa matokeo mazuri ya kidato cha sita mwaka huu na miaka iliyopita na ufaulu mzuri pia hata kwa kidado cha nne na kuwasihi kuendelea kufanya vizuri zaidi ili elimu hiyo iwakomboe wao binafsi na taifa kwa ujumla.

 

Aidha, ametoa wito kwa Viongozi wa Mkoa wa Tabora kuwa karibu na wanafunzi wa shule hiyo na shule nyingine zote ili wawasaidie kukua kimaadili.

 

“Watoto hawa ni wadogo, tuwasaidie hata watakapotoka hapa waendelee kuwa na sifa nzuri huko watakakokwenda.


 







MHE. RIDHIWANI AWAELEKEZA WAAJIRI MKOANI TABORA KUMALIZA CHANGAMOTO ZOTE ZA WATUMISHI MWAKA HUU WA FEDHA

Na. Veronica Mwafisi-Tabora

Tarehe 11 Julai, 2026


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewaelekeza Waajiri katika Sekta ya Umma mkoani Tabora kufanyia kazi madai ya watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha.

 

Akifanya kikao cha majumuisho na Viongozi na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 11 Julai, 2026 baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo, Mhe. Kikwete amesema katika mwaka huu wa fedha Waajiri washughulikie masuala yote ya kiutumishi ikiwemo kupanda madaraja, kulipa malimbikizo, kuwabadilisha kada wanaostahili pamoja na madai mengine.

 

Amesema Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko mbalimbali ya watumishi kuhusiana na kutoshughulikiwa stahiki zao jambo ambalo limekuwa likishusha ari ya utendaji kazi na kushindwa kuwahudumia wananchi kikamilifu.

 

“Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka wananchi wake wapate huduma bora, mwaka huu wa fedha tushughulikie changamoto zote za watumishi ili watoe huduma kwa furaha,” amesisiza.

 

Kuna watumishi wana sifa ya kupandishwa madaraja, wengine kubadilishiwa kada na wengine wana madai yao mbalimbali. “Ninaelekeza wote wanaostahili watekelezewe na kama kuna changamoto yoyote mnayokutana nayo katika utekelezaji wa hili mtuletee Ofisini tuone namna ya kulitatua,” ameongeza

 

Aidha, amewataka Maafisa Rasilimaliwatu kutoa ushauri kwa Waajiri utakaosaidia kutatua changamoto za kiutumishi.

 

Amesema changamoto za kiutumishi zikishindwa kutatuliwa basi wa kulaumiwa si mwingine bali ni Maafisa Rasilimaliwatu kwani wanayo nafasi kubwa ya kutoa ushauri mzuri kulingana na taaluma zao.

 

Mhe. Kikwete amewapongeza Viongozi na Watumishi wa Mkoa huo kwa ushirikiano mzuri baina ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi uliochangia utekelezaji mzuri wa majukumu ya miradi ya maendeleo.

 

 “Tunatekeleza Ilani ya Chama kilichoko madarakani, niwapongeze kwa ushirikiano baina yenu, endeleeni kufanya kazi kwa pamoja kwani ndio msingi wa maendeleo ya taifa letu,” ameongeza

 

Vile vile Waziri Kikwete ametoa wito kwa Viongozi na Watumishi wa Mkoa huo kuzungumza na wananchi ikiwemo vijana na kusikiliza changamoto zao badala ya kusubiria viongozi wengine kutoka maeneo ya mbali kuzungumza.

 

Amesema kujua changamoto za vijana hao kunasaidia kwani wengine unakuta wanahitaji kitu kidogo cha kujiendeleza kiuchumi na kumuepusha kuingia katika masuala yasiyo na maadili.

 

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Bi. Upendo Wella amemshukuru Mhe. Kikwete kwa ziara aliyoifanya katika mkoa huo ambayo itaenda kuboresha utendaji wa Watumishi kwa maendeleo ya taifa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Umma na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Tabora baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.


Sehemu ya Viongozi, Watumishi wa Umma na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Sehemu ya Viongozi na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.


Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Tabora, Viongozi na Watumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

 

Sehemu ya Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Sehemu ya Viongozi na Watendaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

 









 

 

 

Friday, July 10, 2026

MHE. RIDHIWANI ASISITIZA WAAJIRI KUTILIA MKAZO SUALA LA MSAWAZO KWA WATUMISHI ILI KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA UHABA WA WATUMISHI

Na. Veronica Mwafisi-Urambo

Tarehe 10 Julai, 2026

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewakumbusha Waajiri katika Taasisi za Umma kutilia mkazo suala la msawazo kwa Watumishi ili kupunguza changamoto ya uhaba wa watumishi katika maeneo mbalimbali kwenye sekta hiyo ya umma kwa lengo la kuwatumikia wananchi kwa ufasaha.

 

Mhe. Kikwete amesema hayo leo tarehe 10 Julai, 2026 wakati akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha Polisi Usoke.

 

Amesema kabla ya Waajiri kulalamika changamoto ya uhaba wa watumishi, ni vema wakakaa na kufanya msawazo ili kujiridhisha kama kweli wana changamoto hiyo katika maeneo yao kabla ya kuomba kupatiwa watumishi wapya.

 

“Utakuta kuna taasisi watumishi wa kada fulani wamerundikana katika kituo kimoja cha kazi huku kituo cha kazi cha jirani kina uhaba wa watumishi wa kada hiyo, au Waajiri kaeni, fanyeni msawazo, kabla ya kulalamikia changamoto hiyo ya uhaba wa watumishi,” ameongeza Mhe. Kikwete.

 

Ameongeza kuwa kuna taasisi unakuta kuna watumishi wa kada fulani ambao sio hawahitajiki sana katika taasisi fulani kutokana na majukumu yake lakini wapo huku taasisi yenye uhitaji wa watumishi wa kada hiyo hakuna.

 

Katika hatua nyingine Mhe. Kikwete amewataka wananchi wa Kata ya Usoke kukitunza kituo cha Polisi kinachojengwa katika kata hiyo ili kiwasaidie katika kupambana na uhalifu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha Polisi Usoke wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wakwanza kulia) akiwa katika mkutano mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi Usoke, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua ujenzi wa kituo cha Polisi Usoke katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyevaa miwani) akipiga makofi mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi Usoke, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisikiliza taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha Polisi Usoke katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kabla ya kukagua na kuweka jiwe la msingi wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.


Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi Usoke, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.