Na.
Lusungu Helela -Dodoma
Mkurugenzi
Msaidizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Bw. Priscus Tairo ametoa wito kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI
kuchukua muda wao kujifunza kwa undani Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji
Kazi katika Utumishi wa Umma ili kuwa msaada kwa watumishi walio nje ya Ofisi
hiyo ambao wamekuwa wakihitaji kupata mafunzo ya mfumo huo ili waweze
kuutekeleza kwa ufanisi.
Bw.
Tairo ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Disemba 02, 2024 Ofisi ya
Rais-UTUMISHI iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma wakati akitoa
mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Ofisi hiyo, ikiwa ni muendelezo
wa kutoa mafunzo elekezi ya kila wiki kwa Watumishi hao kwa
lengo la kuboresha utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma nchini.
Bw.
Tairo amesema Mfumo huu ni mpya, hivyo unahitaji watumishi wengi wenye uwezo wa
kutoa msaada wa kiufundi kwa ukaribu, haraka na ufanisi ili kuleta matokeo
yaliyokusudiwa.
Amesema
endapo Watumishi wa Ofisi hiyo wataweza kuufahamu vizuri jinsi mfumo huo wa e-
unavyotenda kazi utawawezesha kutoa msaada kwa watumishi wengine wakati wowote
na mahali popote lengo likiwa ni kuifanya Serikali iweze kubaini mwenendo
halisi wa utendaji kazi wa watumishi wa umma nchini.
Kufuatia
hatua hiyo, Bw. Tairo amewataka Watumishi wa Ofisi hiyo kutumia muda
wao mwingi kujinoa katika eneo hilo kwani Watumishi wa nje ya Ofisi hiyo
wana imani kubwa na watumishi wa Ofisi hii bila kujali wanatoka katika
idara inayojihusisha na mafunzo hayo.
Mwakilishi kutoka Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Charles Shija akizungumza mara baada ya kumalizika mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Priscus Tairo akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma kwa Watumishi wa Ofisi hiyo, ikiwa ni muendelezo wa kutoa mafunzo elekezi ya kila wiki kwa Watumishi hao kwa lengo la kuboresha utendaji kazi
Baadhi
ya Watumishi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya
kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika
katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mtumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Dickson Isaya akiwasilisha hoja wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment