Na Mwandishi Wetu - Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Watumishi Housing
Investments (WHI) ni taasisi ambayo imefanya mambo makubwa
kwani tangu kuanzishwa kwake
limeleta mapinduzi makubwa kwa Watumishi wa Umma kuweza kumiliki nyumba
bora kwa masharti nafuu, hatua inayolenga kuboresha hali ya maisha na kuongeza
ufanisi kazini.
Mhe. Simbachawene ametoa
kauli hiyo leo katika eneo la nyumba zilizojengwa na WHI Njedengwa jijini Dodoma wakati akimkaribisha Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa
ajili ya kuzindua Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma.
Mhe. Simbachawene amesema WHI imefanikiwa kutekeleza makazi kwa
Watumishi wa Umma jumla ya nyumba 1006 katika mikoa 19 nchini lengo likiwa ni kutatua changamoto ya makazi inayowakabili Watumishi hao
hususan wa kipato cha chini.
Amesema mpango huo ulibuniwa
ili kuwapa nafuu watumishi kumiliki nyumba hizo ikizingatiwa kuwa katika kipindi cha nyuma haikuwa rahisi kwa watumishi hao kumiliki
nyumba kutokana na makampuni mengi yanayojihusisha na ujenzi wa nyumba kujiendesha kibiashara kwa lengo la kupata faida.
Amesema, shabaha kubwa ya WHI ni kujenga nyumba vijijini kwa ajili ya kuwawezesha watumishi wa kipato cha
chini wakiwemo Walimu na Wauguzi kuweza kumiliki nyumba pamoja na kujenga maeneo ya
mijini ili kuwasaidia watumishi wenye kipato cha chini na ajira mpya kuacha
kupanga nyumba mbali na maeneo yao ya kazi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma, Mhe. Augustine Holle
amesema WHI ni Taasisi ambayo imekuwa ikijenga nyumba zinazouzika tofauti na
Taasisi zingine kutokana na kujenga nyumba hizo kulingana na kipato cha wateja
wake ambao ni Watumishi wa Umma
"WHI ni Taasisi makini
ambayo imejikita kurahisisha umiliki wa nyumba kwa Watumishi wa Umma kuwa
urahisi na endelevu " amesisitiza Mhe. Holle.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa WHI, Dkt. Fred Msemwa amesema suala la makazi kwa Watumishi wa Umma ni jambo
lisiloepukika kwani linachochea ufanisi wa kazi kwa Watumishi hao.
Amesema tangu kuanzishwa kwa
taasisi hiyo wamekuwa wakifanya
jitihada za kujenga nyumba za Watumishi kwa bei rahisi ili kuwawezesha
Watumishi hao kuweza kumiliki nyumba hizo kwa kuzinunua kwa bei rahisi.
"Kwa mara ya kwanza
haikuwa rahisi, nyumba zilizojengwa licha ya kuwalenga Watumishi lakini
walikuwa hawawezi kuzinunua kutokana gharama yake kuwa juu ila kwa sasa
Watumishi wamekuwa wakizifurahia," amesisitiza Dkt. Msemwa.
Utekelezaji wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma ni dhamira pana ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata fursa ya kumiliki makazi bora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) kuzungumza katika halfa hiyo iliyofanyika katika Nyumba za Watumishi, Njedengwa jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi
wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa kwenye
hafla ya ufunguzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma iliyofanyika katika
Nyumba za Watumishi, Njedengwa jijini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango (aliyevaa
tai nyekundu) akiwasili eneo la Njedengwa jijini Dodoma kwenye hafla ya
ufunguzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene pamoja
na Viongozi mbalimbali.
Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akitoa utambulisho wa Viongozi na wageni walioshiriki
kwenye hafla ya ufunguzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi
wa Umma iliyofanyika katika Nyumba za Watumishi, Njedengwa jijini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa pili kutoka
kulia) akiweka jiwe la msingi kwenye hafla ya ufunguzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi
wa Umma iliyofanyika katika Nyumba za Watumishi, Njedengwa jijini Dodoma. Wa nne
kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
na wa pili kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala
Bora, Mhe. Deus Sangu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa kwanza kutoka kushoto)
akizungumza jambo na Viongozi wa mbalimbali. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa ofisi
yake Mhe. Deus Sangu na wa pili kutoka
kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na
Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene wakati akizungumza katika hafla
ya ufunguzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma kabla ya Waziri huyo kumkaribisha
mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip
Mpango (hayupo pichani).
Sehemu ya Wakurugenzi
na Wakurugenzi Wasaidizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi
wa Umma iliyofanyika katika Nyumba za Watumishi, Njedengwa jijini Dodoma.
Wakurugenzi
wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa
kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati meza kuu aliyekaa) wakati wa hafla
ya ufunguzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma iliyofanyika katika Nyumba
za Watumishi, Njedengwa jijini Dodoma.
Sehemu
ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla
ya ufunguzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma iliyofanyika
katika Nyumba za Watumishi, Njedengwa jijini Dodoma.
Mwonekano
wa mfano wa nyumba ya Makazi kwa Watumishi wa Umma iliyopo Njedengwa jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment