Monday, December 23, 2024

WATUMISHI WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU WANAPOTIMIZA WAJIBU WAO

Na. Lusungu Helela -Dodoma

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewataka Watumishi wa Umma kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu huku wakisistizwa kutambua haki zao za msingi wanazostahili kama Watumishi wa Umma.

Afisa Utumishi Mkuu, Bw. Elibariki Funga akiwasilisha mada kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Desemba 23, 2024 katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma wakati akitoa  mafunzo ya haki na wajibu kwa  Watumishi wa Umma nchini,  ikiwa ni muendelezo wa kutoa mafunzo elekezi ya kila wiki kwa Watumishi  hao  kwa  lengo la  kuboresha utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma nchini.

Amesema ni wajibu wa kila Mtumishi kutambua haki zake ikiwemo stahili zake kama Mtumishi wa Umma pamoja na likizo huku akisisitiza haki lazima iende sambamba na kutimiza wajibu wa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema endapo Watumishi wa Ofisi hiyo wataweza kufahamu vizuri haki zao wataweza kuwajibika ipasavyo ili kuendana na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Afisa Utumishi Mkuu, Bw. Elibariki Funga (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu Haki katika Utumishi wa Umma wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora yanayofanyika kila Jumatatu katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (wa kwanza kushoto) akifuatilia wasilisho kuhusu Haki katika Utumishi wa Umma wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora yanayofanyika kila Jumatatu katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli (aliyesimama) akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora yanayofanyika kila Jumatatu katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Wengine ni Wakurugenzi wa Idara na vitengo mbalimbali wa ofisi hiyo.


Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Umma, Bi. Felista Shuli akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora yanayofanyika kila Jumatatu katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Bi. Hilda Kabisa (aliyesimama) akijibu hoja kuhusu sheria wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao kuhusu Haki katika Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Afisa Utumishi Mkuu kutoka ofisi hiyo Bw. Elibariki Funga (hayupo pichani) wakati akiwasilisha mada kuhusu Haki katika Utumishi wa Umma kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.








No comments:

Post a Comment