Sunday, December 8, 2024

MHE. SIMBACHAWENE AWAJULIA HALI WABUNGE MAJERUHI WALIOPATA AJALI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewajulia hali baadhi ya Wabunge majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao walipata ajali ya gari Mkoani Dodoma wakati wakielekea kwenye Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mombasa Nchini Kenya Desemba 6, 2024.

Waziri Simbachawene ametoa pole kwa majeruhi hao na kuwatakia uponyaji wa haraka ili waweze kurudi katika majukumu yao ya kila siku.

Aidha, Mhe. Simbachawene aliongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson ambaye pia alienda kutoa pole kwa Wabunge hao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimjulia hali mmoja wa Wabunge majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson.

No comments:

Post a Comment