Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Mb) amesema maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kwa mwaka 2024 yamekuja na fursa ya Kongamano mahususi kwa ajili ya Watumishi wa Umma kujitathmini ni kwa namna gani wanawajibika kwa Umma na kutekeleza jukumu la Serikali la Ustawi wa Wananchi kwa kuzingatia Haki za Binadamu na kuepuka vitendo vya rushwa.
Mhe. Simbachawene amesema hayo Disemba 5, 2024 katika Ukumbi wa
NAOT Dodoma wakati akiongea na Waandishi
wa Habari katika uzinduzi wa siku ya maadili na haki za binadamu.
“Ninaamini, Watumishi wa Umma watatumia fursa ya uwepo wa
Kongamano hilo kujitathmini kuhusu uzingatiaji wa Haki za Binadamu na kuepuka
rushwa wanapotoa huduma kwa Umma”. alisema Mhe. Simbachawene.
Aidha, katika Kongamano hilo, zitawasilishwa na kujadiliwa mada
mbili ambazo ni Haki za Binadamu katika Mapambano Dhidi ya Rushwa” na “Maadili,
Haki na Wajibu wa Watumishi wa Umma. Mada hizo zimezingatia Kaulimbiu ya mwaka
2024 isemayo “Tumia haki yako ya Kidemokrasia, chagua viongozi waadilifu na
wanaozingatia Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora kwa maendeleo ya
Taifa letu”
Sambamba na Kongamano hilo, Taasisi Simamizi za Utawala Bora
zitafanya ziara kwenye Magereza ya Kongwa na Mpwapwa Mkoani Dodoma na
kuwasikiliza wafungwa na mahabusu na
kutoa misaada ya kijamii.
Kila tarehe 10 Desemba, Tanzania huungana na nchi nyingine Duniani
kuadhimisha Siku ya Haki za Binadamu Kimataifa ikiwa ni utekelezaji wa Tamko la
Haki za Binadamu liililopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, tarehe 10
Desemba, 1948 (Universal Declaration of
Human Rights - UDHR).
Taasisi zinazoshirikiana katika kuadhimisha Siku ya Maadili na
Haki za Binadamu Kitaifa ni pamoja na Ofisi ya Rais, Ikulu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Katiba na Sheria,
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa, Tume ya Utumishi wa Umma, Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma, Ofisi
ya Taifa ya Ukaguzi, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Ofisi ya
Mkaguzi Mkuu wa Ndani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza
na Waandishi wa Habari na Viongozi wa Taasisi Simamizi za Maadhimisho
katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati)
akifuatilia jambo wakati akizundua maadhimisho
ya siku ya maadili na haki za binadamu jijini Dodoma. Kulia kwake ni Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula
Mahendeka.
Mwenyekiti
wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe.Jaji (Mst) Hamisa Kalombola (katikati) akimsikiliza
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizindua maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu jijini Dodoma.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bi.
Neema Mwakalyelye akifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
(hayupo pichani) kuhusu uzinduzi wa maadhimisho
ya siku ya maadili na haki za binadamu jijini Dodoma.
Viongozi na Watendaji wa Taasisi
Simamizi za Maadhimisho wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
(hayupo pichani) kuhusu uzinduzi wa maadhimisho
ya siku ya maadili na haki za binadamu jijini Dodoma.
Viongozi na Watendaji wa Taasisi
Simamizi za Maadhimisho wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
(hayupo pichani) kuhusu uzinduzi wa maadhimisho
ya siku ya maadili na haki za binadamu jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment