Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewaasa wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kutumia vyema taaluma na ujuzi waliopata kwa manufaa yao na taifa kwa jumla.
Mhe. Simbachawene amesema hayo leo
katika sherehe za Mahafali ya 40
ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali katika Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
“Kuhitimu ngazi za Shahada, Stashahada,
Astashahada na Astashahada ya Awali katika fani mbalimbali sio jambo dogo,
elimu mliyopata ni kubwa, tumieni elimu hiyo kwa manufaa yenu na ustawi wa
taifa” alisema Mhe. Simbachawene.
Aliongeza kuwa, ukuaji wa taifa lolote unategemea
uwepo wa rasilimaliwatu imara na yenye weledi wa kutosha. Hivyo, amewataka wahitimu
hao, kuepuka rushwa, ufisadi na kujikinga na ugonjwa hatari wa UKIMWI na
magonjwa mengine yasiyoambuza kwa kuwa Taifa linawahitaji kwa ustawi imara.
Ameongeza kuwa, kuhitimu katika fani
yoyote ile ni matokeo ya jitihada za muda mrefu si kwa wahitimu wenyewe tu bali
pia hata kwa wale waliowasaidia kufikia hatua hiyo ikiwa ni pamoja na walimu,
wazazi na walezi.
Vilevile,
ameueleza Uongozi wa chuo kutambua kuwa Serikali ina matarajio makubwa na Chuo
hicho hasa katika kuwajengea uwezo watumishi wa Umma na kutoa wahitimu wenye
umahiri, uzalendo na tabia njema na hivyo kujenga uchumi wa nchi endelevu.
Awali,
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Ernest
Mabonesho alimshukuru Mhe. Simbachawene kwa kukubali mwaliko wao na kumtarifu
kuwa pamoja na jitihada nyingine zinazofanywa na chuo pia, chuo kimeendelea na
juhudi za kufufua na kuanzisha ushirikiano na taasisi mbalimbali ndani na nje
ya nchi kwa lengo la kuboresha ujuzi na kubadilishana uzoefu.
“Ili
kuboresha mafunzo yetu, tumeona hainabudi kushirikiana na vyuo vingine vya nje na
ndani ya nchi hususani vinavyohusika na masuala ya Utumishi wa Umma ili kuweza
kupata fursa ya kujifunza na kutoa mafunzo bora zaidi” alisema Dkt. Mabonesho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza
na wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo
pichani) katika mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania yaliyofanyika katika
Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Sehemu ya wahitimu wa kozi
mbalimbali katika mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakiwa kwenye
maandamano yaliyofanyika nje ya Ukumbi wa Mkapa jijini
Mbeya.
Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akitoa neno
la utangulizi kwa wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo pichani) kabla
ya
kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
kuzungumza
na wahitimu hao wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika
katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Sehemu ya Wahitimu wa Astashahada, Stashahada
na Shahada ya kozi mbalimbali wakiwa
wamesimama baada ya kutambulishwa kwa mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
(hayupo pichani) kabla ya Waziri huyo kuzungumza nao kwenye mahafali ya 40
ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
yaliyofanyika katika
Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Mtendaji Mkuu na
Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho
akiwasilisha taarifa ya utendaji wa chuo
kwa mgeni rasmi Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene wakati
wa mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyevaa kofia nyekundu) akijumuika
kwenye maandamano yaliyofanyika nje ya
Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya wakati wa mahafali
ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu na
Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho na
kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo hicho Dkt. Dkt.
Frolens Turuka.
Sehemu ya Wahitimu wa Astashahada,
Stashahada
na Shahada ya kozi mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene (hayupo pichani) wakati
wa mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika
Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Baadhi
ya watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania na wageni waalikwa waliohudhuria
mahafali ya 40 ya Chuo
cha Utumishi wa Umma Tanzania wakifuatilia
hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene katika
Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Sehemu
ya Wazazi na wageni waliohudhuria mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene katika
Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene (aliyevaa kofia nyekundu) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu
wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania waliofanya vizuri wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo hicho
yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. Wengine ni Viongozi
na Watendaji mbalimbali
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene akicheza nyimbo ya kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania iliyokuwa ikizungumzia utendaji kazi mzuri wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika
Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Vijana
wa kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakitumbuiza kwenye mahafali ya 40 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika
Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment