Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 03 Desemba, 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amemtaka Mkandarasi SUMA JKT anayejenga ofisi
ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kukamilisha haraka ujenzi wa jengo la
ofisi hiyo kwa mujibu wa mkataba kwa kuwa eGA ni kiini cha uendeshaji wa Serikali
katika kujenga mifumo imara itakayoboresha utoaji wa huduma Serikalini.
Mhe. Simbachawene amesema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi hiyo jijini Dodoma.
“eGA ni kiini cha uendeshaji wa Serikali mtandao hivyo, tuna wajibu wa kurahisisha utendaji
kazi wa taasisi za Serikali kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa kwa
wananchi, hivyo tumieni nguvu nyingi kukamilisha
ujenzi huu kwa mujibu wa mkataba na kwa wakati,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mkuu, Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA)
Mhandisi Benedict Ndomba amesema, Serikali ya
Awamu ya Sita kipaumbele chake kikubwa ni kuwa na Serikali ya Kidijitali ili
kutoa huduma bora na kwa wakati, hivyo kukamilika kwa jengo hilo kwa wakati
kutaisaidia Serikali kufikia malengo yake ya kujenga mifumo imara
itakayoboresha utoaji wa huduma Serikalini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi hiyo jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba (wa sita kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyevaa tai nyekundu) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi na Watendaji mbalimbali.
Mwakilishi kutoka ofisi ya Mshauri elekezi (TBA),
Bw. Tsere Willium (aliyenyanyua mkono) akimweleza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
(wa kwanza kulia) maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao
(eGA) unaoendelea wakati Waziri
huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo
jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akielekea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) unaoendelea jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Rais-IKULU, Bi. Ened Munthali (kulia)
akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua
maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) unaoendelea jijini
Dodoma.
Mwonekano wa jengo la ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA)
linaloendelea kujengwa jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment