Na. Veronica Mwafisi
Tarehe 16 Desemba, 2024
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, wamesisitizwa kuzingatia uandishi wa Nyaraka za
Serikali ikiwemo barua, dokezo na taarifa mbalimbali ili kurahisisha
mawasiliano ndani ya ofisi baina ya Idara na Vitengo.
Mchambuzi
kazi, Idara ya Usimamizi wa Taasisi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora,
Bw. Macdonald Kiwia ameyasema hayo leo tarehe 16 Desemba, 2024 wakati
akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo wa Uandishi wa Nyaraka mbalimbali za Serikali wakati wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi na Watumishi
wa ofisi katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini
Dodoma.
Aidha, Bw. Kiwia ametoa wito kwa watumishi hao kuzingatia Sheria, Kanuni Taratibu na Miongozo mbalimbali ya uandishi wa Nyaraka za Serikali ili kuboresha utendajikazi kwa watumishi hao na watumishi wa umma nchini kote.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala
na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bw. Musa Magufuli amewasisitiza watumishi wa ofisi
hiyo kuhudhuria mafunzo hayo bila kukosa kila siku ya Jumatatu kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi wote na kuwa na uelewa wa pamoja wa matumizi
sahihi ya masuala mbalimbali kuhusu Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala
na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo wakati akihitimisha mafunzo
yaliyolenga kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya Uandishi wa Nyaraka
za Serikali yaliyofanyika katika ofisi hiyo
iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma, Bw. Juma Mkomi (mstari wa pili, wa tatu kutoka kulia) akifuatilia
mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo
Viongozi na watumishi wa ofisi hiyo kuhusu masuala ya Uandishi wa Nyaraka za
Serikali yaliyofanyika katika Mji wa
Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mchambuzi kazi, Idara ya Usimamizi
wa Taasisi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Macdonald Kiwia
akiwasilisha mada kuhusu viwango mahsusi vya uandishi wa dokezo wakati wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi na watumishi wa ofisi
hiyo kuhusu masuala ya Uandishi wa Nyaraka za Serikali yaliyofanyika katika Mji wa
Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia mada mbalimbali kuhusu Uandishi wa Nyaraka za Serikali wakati wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo
Viongozi na watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia
mada mbalimbali kuhusu Uandishi wa Nyaraka za Serikali wakati
wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi na watumishi wa ofisi
hiyo yaliyofanyika katika Mji wa
Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea
uwezo watumishi hao kuhusu Uandishi wa Nyaraka za Serikali yaliyofanyika katika ofisi hiyo
iliyopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment