Sunday, December 8, 2024

WAZIRI SIMBACHAWENE: TAFITI KUIMARISHA UTENDAJIKAZI SERIKALINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amesema tafiti mbalimbali zinazofanyika nchini zikiwafikia wadau zitasaidia kuimarisha mifumo ya utendajikazi katika utumishi wa umma.

Mhe. Simbachawene amesema hayo katika sherehe za Mahafali ya 40 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Tafiti hizo zilizofanywa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ni mpango wa kuendeleza Chuo hicho ili kufikia malengo na azma ya Serikali na maelekezo yanayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kusimamia nchi ambazo zitasaidia kuimarisha ustawi wan chi.

Aidha, Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa chuo hicho kuendelea kufanya tafiti tumizi ili kuzifanya zitumike na kuhakikisha zinawafikia wadau ili waweze kuzisoma na kuchambua kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali kwani tafiti hizo ni uwekezaji muhimu hasa katika masuala ya uongozi na utumishi yanayogusa masuala ya kila wananchi.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza kabla ya kuzindua tafiti mbili zilizofanywa na Chuo cha Utumishi wa Umma wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tafiti mbili zilizofanywa na Chuo cha Utumishi wa Umma wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa chuo hicho, Dkt. Florens Turuka.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) akimpatia kitabu Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (wa kwanza kushoto) kinachohusu tafiti mbili zilizofanywa na Chuo cha Utumishi wa Umma wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.


Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Florens Turuka (aliyesimama) akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzindua tafiti mbili zilizofanywa na Chuo cha Utumishi wa Umma wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.



No comments:

Post a Comment