Na. Lusungu Helela- Dodoma
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amesema Wananchi walio
wengi wamekuwa wakitumia mitandao ya Kijamii kufikisha malalamiko yao kwenye
Taasisi za Serikali kutokana na baadhi ya Watumishi wa Umma
kuvujisha siri za wateja wao pindi wananchi hao wanapotumia mifumo rasmi kutoa
mrejesho
Amesema vitendo hivyo vimekuwa vikiwakatisha tamaa
Wananchi wenye nia njema ya kuona Serikali inakuwa kinara wa kutoa huduma bora
kwa wananchi wake.
Bw. Daudi ametoa kauli hiyo leo Jumanne Disemba 3,
2024 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa
Mrejesho kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za
Umma
Amewataka Maafisa hao kutunza siri za wateja wao ili
kuwafanya Wananchi kuwa huru kuwasilisha changamoto zinazowakabili wakati
wowote na mahali popote pasipo kulazimika kutumia mitandao ya kijamii
Bw. Daudi ameongeza kuwa Mfumo wa e-Mrejesho
unampa fursa mwananchi kutuma malalamiko, pongezi pamoja na
maulizo kwa Serikali mahali popote na wakati wowote.
Kufuatia hatua hiyo Bw. Daudi amewataka Maafisa hao
mara baada ya kurudi katika vituo vyao vya kazi wakahakikishe wanakuwa
waadilifu na wenye kutunza siri za ofisi na za wateja wao ili
kuwafanya wananchi kuwasilisha malalamiko yao kwenye njia rasmi
Aidha, Bw. Daudi amewataka Maafisa hao wakaimarishe
Madawati au Ofisi za Mrejesho zilizopo katika Taasisi zao ili kufanikisha
ushughulikiaji mrejesho kwa ufanisi na kwa wakati katika Ofisi za Umma kwa
vile wameaminiwa kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usimamzi wa Utawala Bora
kutoka USAID/PS3+ awamu ya pili Dkt. Emmanuel Malangalila amesema
wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha mfumo
huo unatumika ipasavyo katika Serikali za Mitaa ambako ndiko kuna malalamiko
makubwa kutoka kwa wananchi .
Mafunzo haya yanalenga kuona huduma zinazotolewa na
Serikali zinafurahiwa na wananchi wote bila kujali rangi, kabila, mahali au
hali yao ya kiuchumi waliyonayo amesisitiza Dkt. Malangalila
Hivi karibuni Tanzania ilipewa tuzo ya Kimataifa
ya ubunifu wa mfumo ya kidijitali wa Mrejesho (e-Mrejesho) nchini Korea Kusini
na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa Mkutano wa Umoja wa Jukwaa la
Umoja wa Mataifa la Tuzo za Utumishi wa Umma (2024 UN Public Service Awards
(UNPSF) kutokana na umadhubuti wake.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akizungumza na Maafisa Mrejesho jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Mrejesho mara baada ya kufungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akisalimiana na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala Bora kutoka USAID/PS3+ , Dkt. Emmanuel Malangalila mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma, Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavila
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala Bora kutoka USAID/PS3+ , Dkt. Emmanuel Malangalila akizungumza na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavila mara baada ya kuwasili kwenye mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavila akizungumza na Maafisa Mrejesho jijini Dodoma kabla Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi kufungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akiwa kwenye meza kuu na baadhi ya Wakurugenzi mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma, Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavila
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akiwa na baadhi ya Wakurugenzi mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Waratibu wa Mrejesho
No comments:
Post a Comment