Na. Lusungu
Helela- Dodoma
Amewataka wakawe waaminifu na wenye haiba
inayokubalika na Wateja wa ndani na nje
ya Taasisi ili kuwafanya Wateja wao kuwa
huru kufikisha malalamiko yao bila ya kuwa na wasiwasi wa aina yeyote.
Bi.Mavika ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo maalum
yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu kwa Waratibu wa Kushughulikia
Mrejesho kuhusu uendeshaji wa mfumo wa
e-Mrejesho katika Ofisi za Umma.
Bi.Mavika mewataka Waratibu hao kutoa fursa sawa
kwa wananchi wote kwa kutumia mfumo wa e-Mrejesho ili kuwawezesha wateja kutuma
malalamiko, pongezi pamoja na maulizo kwa Serikali mahali popote na
wakati wowote.
Aidha, Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu,UTUMISHI,
Bi.Mavika amewaonya Waratibu hao kuacha tabia ya kushughulikia mrejesho wa
wananchi mara tu wanaposikia kuna ukaguzi maalum kutoka Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
" Nendeni mkawe kioo fanyeni kazi muda wote,
hatutegemei kuona mnashughulikia mrejesho kutoka wananchi mara tu mnaposikia
kuna ukaguzi maalum" amesisitiza Bi.Mavika.
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi.
Janeth Mishinga ameeleza kuwa licha ya Waratibu hao kupewa mafunzo hayo ya
kushughulikia mrejesho kwa wananchi kwa wakati pia wamepewa mafunzo ya
mbalimbali ya kuwafanya kuwa Watumishi wa mfano katika jamii
Naye Mwenyekiti wa Waratibu wa kushughulikia
Mrejesho, Denis Gondwe akizungumza kwa niaba ya Waratibu hao amesema mafunzo
hayo yamekuwa ni muhimu sana kwao ikizingatiwa kuwa shabaha ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya
Uongozi wa Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kutoa huduma bora kwa wananchi
wote bila ubaguzi wa aina yoyote.
Mwakilishi wa Katibu
Mkuu, UTUMISHI, Bi.Leila Mavika
akizungumza na Waratibu wa Kushughulikia Mrejesho jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo maalum yaliyofanyika
kwa muda wa siku tatu kwa Waratibu hao kuhusu
uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma
Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Janeth Mishinga akizungumza na Maafisa Mrejesho jijini Dodoma kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bi.Leila Mavika kufunga mafunzo maalum ya siku tatu kwa Waratibu hao kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma
Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Janeth Mishinga akiwa ameongoza na Mwakilishi wa Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bi.Leila Mavika akiwasili kwa ajili ya kufunga mafunzo maalum ya siku tatu kwa
Waratibu wa kushughulikia Mrejesho kuhusu
uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bi.Leila Mavika (katikati) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Janeth Mishinga kabla ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bi. Leila Mavika ya kufunga mafunzo maalum ya siku tatu kwa Waratibu hao kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma, wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Waratibu wa kushughulikia Mrejesho, Denis Gondwe
Baadhi ya Waratibu wa Kushughulikia Mrejesho wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bi.Leila Mavika akizungumza nao leo jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo maalum yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu kwa Waratibu hao kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma
Mwezeshaji wa mafunzo kwa Waratibu wa kushughulikia Mrejesho, Bw. Hassan akizungumza Waratibu wa Kushughulikia Mrejesho jijini Dodoma kabla ya Mgeni rasmi Mwakilishi wa Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bi. Leila Mavika kufunga mafunzo maalum yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu kwa Waratibu hao kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma
No comments:
Post a Comment