Na. James K. Mwanamyoto-Kazuramimba
Tarehe 23 Desemba, 2021
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa amewataka Waratibu wa TASAF nchini kuhakikisha walengwa
wanapewa ruzuku kabla ya Sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya ili waweze kujipanga
mapema kuboresha maisha yao.
Akizungumza
na wananchi na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Kazuramimba, Halmashauri ya
Wilaya ya Uvinza, Waziri Mchengerwa amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
alishatoa maelekezo ya kuwapatia ruzuku walengwa wa TASAF mara baada ya
kukamilika kwa zoezi la uandikishaji na uhakiki.
“Waratibu
wa TASAF hakikisheni walengwa wa Kazuramimba wanalipwa kwa wakati kabla ya
Krismasi ili wapange mikakati madhubuti itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi
katika Mwaka Mpya unaokuja,” Mhe.
Mchengerwa amesisitiza.
Akizungumzia
azma ya Serikali ya kuwahudumia wananchi, Mhe. Mchengerwa amesema, Serikali
isiyowajali walengwa wa TASAF ni sawa na Serikali isiyokuwa na huruma kwa
wananchi wake na kukosa hofu ya Mwenyezi Mungu.
Mhe.
Mchengerwa ameongeza kuwa, dhamira ya Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu
Hassan ni kuzifikia kaya milioni moja na laki tano ambazo ni sawa na Watanzania
milioni kumi na tano ambao watanufaika na mpango wa kuzinusuru kaya zenye
uhitaji.
Waziri
Mchengerwa amesema, Baba wa Taifa alisema kama Taifa hatutaweza
kupiga hatua iwapo Watanzania wengi wana hali duni
ya maisha na ndio maana Serikali ya Awamu ya Sita imeamua
kuzikwamua kaya zisizojiweza kupitia mpango wa TASAF.
Katika
kuhakikisha miradi ya TASAF inatekelezwa ipasavyo, Mhe. Mchengerwa amesema akiwa
ndiye Waziri mwenye dhamana ya kumsaidia Mhe. Rais kusimamia utekelezaji wa miradi
ya TASAF, atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kutimiza azma ya Mhe.
Rais kuzifikia kaya zote zenye hali duni nchini.
Mhe.
Mchengerwa amehitimisha ziara ya kikazi mkoani Kigoma yenye lengo la kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha
Kazuramimba, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza akiwa kwenye ziara ya kikazi ya
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Kigoma.
Baadhi ya wananchi na walengwa wa TASAF
wa Kijiji cha Kazuramimba wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa
alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji
wa miradi ya TASAF katika Kijiji hicho Mkoani wa Kigoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna wa Polisi Mhe.Thobias Andengenye akitoa neno la
utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa kuzungumza na
wananchi wa Kazuramimba wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa
miradi ya TASAF mkoani Kigoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akielekea
kukagua miradi ya TASAF iliyopo Kijiji cha Kazuramimba, akiwa na viongozi, watendaji
na baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho
wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani
Kigoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akisikiliza ushuhuda wa mlengwa wa TASAF, Bi. Hija
Kaziyabure wa Kijiji cha Kazuramimba, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza wakati
akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Mkoani Kigoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akimpongeza mlengwa wa TASAF, Bi. Tamasha Zegeli wa Kijiji
cha Kazuramimba, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza kwa matumizi mazuri ya ruzuku
ya TASAF wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF katika Mkoa wa Kigoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akicheza
ngoma na wasanii wa kikundi cha Mapigo Tisa cha Kazuramimba mara baada ya
kuwasili Kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi na walengwa wa TASAF
akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
No comments:
Post a Comment