Na. James K.
Mwanamyoto-Kigoma
Tarehe 21 Desemba, 2021
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema
TASAF imejenga nyumba ya Mganga katika Kijiji cha Kagongo, Halmashauri ya
Wilaya ya Kigoma kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati
katika Zahanati ya kijiji hicho.
Akizungumza na wananchi na
walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Kagongo, Mhe. Mchengerwa amesema, ujenzi wa
nyumba hiyo umewaondolea adha wananchi wa kijijiji hicho ya kuchelewa kupata
huduma kwani Mganga aliyekuwa akiwahudumia alilazimika kusafiri takribani
kilomita kumi kila siku ili kutoa huduma kwa wananchi wa kijiji hicho.
“Tumefanikisha ujenzi wa
nyumba hii, Mganga anaishi hapa na huduma zinatolewa kwa wakati, hii ndio
dhamira ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwasogezea huduma wananchi,” Mhe.
Mchengerwa amesisitiza.
Mhe. Mchengerwa ameongeza
kuwa, Serikali kupitia TASAF itaendelea kuboresha huduma za kijamii ili
wananchi waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na Serikali yao kama ambavyo
Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Samia Suluhu Hassan amedhamiria.
Katika kuhakikisha dhamira
hiyo inatekelezwa, Mhe. Mchengerwa amesema, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
ametoa fedha za kutosha kuwezesha upatikanaji wa huduma za kijamii katika
maeneo yote yenye uhitaji.
“Nataka niwatoe hofu
Watanzania wenzangu waliokuwa wanafikiri mradi huu wa TASAF hautaendelea,
napenda niwaambie kuwa, Rais wetu ametupatia kiasi cha shilingi trilioni 2.03
kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya TASAF, hii ina maana kuwa, tutazifikia
kaya zote maskini nchini ambazo hazikufikiwa na mpango katika awamu zilizopita,”
Mhe. Mchengerwa ameongeza.
Mhe. Mchengerwa anaendelea na
ziara ya kikazi mkoani Kigoma ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akimpongeza mlengwa wa TASAF, Bw. Luciano Miheze wa Kijiji
cha Kagongo, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa matumizi mazuri ya ruzuku ya TASAF
wakati wa ziara yake ya kikazi ya
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Kigoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akilakiwa na
wananchi na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Kagongo, Halmashauri ya Wilaya ya
Kigoma, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF mkoani Kigoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha
Kagongo, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma mbele ya nyumba ya Mganga wa Zahanati
ya Kijiji cha Kagongo iliyojengwa na TASAF, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Kigoma.
Umati wa wananchi na walengwa wa TASAF
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Kigoma.
Baadhi ya wananchi na walengwa wa TASAF wa
Kijiji cha Kagongo, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wakiwa kwenye mkutano wa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Mchengerwa ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Kigoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akisikiliza ushuhuda wa mlengwa wa TASAF, Bw. Luciano Miheze
wa Kijiji cha Kagongo, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wakati akiwa kwenye
ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa
Kigoma.
No comments:
Post a Comment